Chiriku

(Elekezwa kutoka Fringillidae)
Chiriku
Chiriku wa Kanari
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Fringillidae (Ndege walio na mnasaba na chiriku)
Ngazi za chini

Jenasi 35:

Chiriku ni ndege wadogo wa familia Fringillidae. Spishi bila rangi kali kama njano na nyekundu huitwa mpasuambegu pia na spishi yenye domo nene huitwa yombeyombe. Spishi nyingi zina rangi ya kahawa pamoja na nyeupe na pengine njano au nyekundu na zina michirizi myeusi. Spishi nyingine zina rangi kali kama njano, nyekundu, kijani na/au buluu. Hawa ni ndege wa maeneo yenye miti, lakini wengine wanatokea maeneo wazi na hata majangwa. Hula mbegu lakini hulisha makinda yao wadudu. Hujenga tago lao kwa manyasi, nyuzinyuzi na pengine vigoga na kuvumwani katika panda ya mti. Jike huyataga mayai 2-10.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri