Msingwe

Ndege mkubwa kiasi wa maji wenye rangi ya kahawa
Msingwe
Msingwe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama wari)
Familia: Scopidae (Ndege walio na mnasaba na msingwe)
Jenasi: Scopus
Brisson, 1760
Spishi: S. umbretta
Gmelin, 1789
Ngazi za chini

Nususpishi 4:

Msingwe au mnguri ni ndege mkubwa kiasi na spishi pekee ya jenasi Scopus na familia Scopidae. Umbo wa kichwa chake chenye domo refu na ushungi nyuma yake unakupa ono la nyundo, asili ya jina la ndege huyu kwa Kiingereza (hamerkop). Anatokea Afrika kusini kwa Sahara katika maeneo manyevu kama vile mito na milango yao, maziwa na mabwawa. Hula vyura, samaki na wadudu.

Ndege hawa hujenga kiota kikubwa sana kinachofunikwa kwa mwitiko na kilicho na mwingilio upande. Kiota kina miingilio bandia kadhaa ili kudanganya maadui, kama nyoka na tai. Jike huyataga mayai 3-7.

Nususpishi hariri

Picha hariri