Msingwe
Ndege mkubwa kiasi wa maji wenye rangi ya kahawa
(Elekezwa kutoka Scopidae)
Msingwe | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nususpishi 4:
|
Msingwe au mnguri ni ndege mkubwa kiasi na spishi pekee ya jenasi Scopus na familia Scopidae. Umbo wa kichwa chake chenye domo refu na ushungi nyuma yake unakupa ono la nyundo, asili ya jina la ndege huyu kwa Kiingereza (hamerkop). Anatokea Afrika kusini kwa Sahara katika maeneo manyevu kama vile mito na milango yao, maziwa na mabwawa. Hula vyura, samaki na wadudu.
Ndege hawa hujenga kiota kikubwa sana kinachofunikwa kwa mwitiko na kilicho na mwingilio upande. Kiota kina miingilio bandia kadhaa ili kudanganya maadui, kama nyoka na tai. Jike huyataga mayai 3-7.
Nususpishi
hariri- Scopus umbretta bannermanni, Msingwe Mashariki
- Scopus umbretta minor, Msingwe Mdogo
- Scopus umbretta tenuirostris, Msingwe wa Madagaska
- Scopus umbretta umbretta, Msingwe wa Kawaida
Picha
hariri-
Msingwe kwa karibu
-
Msingwe akila chura-kucha
-
Msingwe akiruka na kifaa cha kujenga kiota
-
Kiota cha msingwe