Mto Goulbi de Maradi

Mto Goulbi de Maradi ni mto unaopatikana kusini ya kati ya Niger na kaskazini ya kati ya Nigeria.

Mto Goulbi de Maradi

Chanzo chake huanzia karibu na Katsina nchini Nigeria na kuishia kwenye mto Rima. Mto huo umbali wake hauzidi kilomita 48 kutoka Niger hadi kwenye mipaka ya Nigeria.

Mto huo ni muhimu sana sababu unatumika kwa kilimo pamoja na umwagiliaji. Mto hupita katika miji ya Niger ambayo ni Maradi, Goudan Roumdji na Madarounfa.

Mto Goulbi de Maradi ni mto wa msimu na unapatikana sana kipindi cha mvua nyingi.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  • Goulbi De Maradi river readings at Madarounfa, 1954-1977, UNESCO.
  • Suttie, J.M., The agro-pastoral potential of the Goulbi de Maradi and the El Fadama River Basins (Niger). FAO - AGO;ESP. Maradi (Niger), Jan 1985
  • Schembri, H., Measurement of the pressure and conductivity of the waters of the phreatic system of the upper cretaceous and quaternary water tables in the Goulbi de Maradi and El Fadama basins. FAO - AGO;ESP. Maradi (Niger), Jan 1985
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Goulbi de Maradi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.