Mji

(Elekezwa kutoka Miji)

Mji ni mkusanyiko wa makazi ya watu, shule, hospitali, ofisi, maduka, viwanda n.k. ulio mkubwa kuliko ule wa kijiji. Mji ukizidi kukua unakuja kuitwa pia jiji.

Mji bora unahitaji mpangilio mzuri wa makazi.

Sura maalumu ya miji inategemea mambo mengi, kuanzia mazingira asili (kama yana milima, mabonde, mito, bandari n.k.).

Miji ya kwanza ilipatikana Mesopotamia, kama vile Uruk na Ur, ingawa kati ya miji inayodumu hadi leo ule wa kale zaidi labda ni Yeriko (Palestina).

Ukuaji wa madola ulifanya baadhi ya miji ipewe hadhi ya mji mkuu, kama vile Roma ambao wakati wa Yesu ulikuwa na wakazi zaidi ya nusu milioni.

Miji yenye wakazi wengi kuliko mingine ni Chongqing, Tokyo, Shanghai, Jakarta, Faiyumna na Varanasi n.k.

Africa ina miji mingi muhimu: Cairo, Lagos, Kinshasa, Johannesburg n.k.

Hadhi ya miji kufuatana na idadi ya wakazi

hariri

Kimataifa kulikuwa na makubaliano kwenye mkutano wa kimataifa ya takwimu ya mwaka 1887 ya kuhesabu kila mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 kama "mji mkubwa", miji kati ya wakazi 20,000 na 100,000 kama miji ya wastani na miji kati ya wakazi 5,000 na 20,000 kama miji midogo. Kufuatana na hesabu hii kulikuwa na miji mikubwa 1,700 duniani wakati wa mwaka 2002.

Katika Tanzania lugha inayotumiwa kisheria [1]ni

 • Jiji ("city") kwa miji mikubwa sana
 • Manisipaa ("municipality") kwa miji ya wastani
 • Mji ("town") kwa miji midogo.

Mkuu wa mji huitwa mwenyekiti kwenye ngazi ya mji wa kawaida, na meya kwenye ngazi za manisipaa na jiji. Wanaongoza mikutano ya Halmashauri ya mji husika.

Marundiko ya mji makubwa barani Afrika

hariri
 1. Lagos, Nigeria milioni 21.0
 2. Cairo, Misri milioni 20.4
 3. Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo milioni 13.3
 4. Luanda, Angola milioni 6.5
 5. Nairobi, Kenya milioni 6.5
 6. Abidjan, Ivory Coast milioni 4.7
 7. Addis Ababa, Ethiopia milioni 4.6
 8. Johannesburg, Afrika Kusini milioni 4.4

Marejeo

hariri
 1. Tanzania LOCAL GOVERNMENT (URBAN AUTHORITIES) ACT, 1982 Archived 10 Januari 2017 at the Wayback Machine., fungu 5,4

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.