Mekong (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Mekong)

Mto Mekong ni kati ya mito mikubwa ya dunia na mto mkubwa wa tatu wa bara la Asia. Mkondo wake ni mkondo mkubwa wa kumi duniani.

Mto Mekong
Mto Mekong wakati wa jioni
Chanzo Tibet, China
Mdomo Bahari ya Kusini ya China
Nchi Tibet
China
Myanmar
Laos
Uthai
Kambodia
Vietnam
Urefu 4,425 km
Kimo cha chanzo 5,200 m
Mkondo 15,000 m³/s
Eneo la beseni 795,000 km²
Miji mikubwa kando lake Vientiane, Phnom Penh

Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Tibet kwenye kimo cha zaidi ya mita 5,000. Mwendo wake una urefu wa zaidi ya km 4000 na beseni ina eneo la kilomita za mraba 795,000.

Kutoka chanzo katika milima ya Himalaya (Tibet) mto unapita jimbo la Yunnan (China) ukijulikana kama Meigong kwa Kichina. Halafu unakuwa mpaka wa Myanmar na Laos. Baada ya km 200 unakutana na tawimto Ruak kwenye eneo linaloitwa "pembetatu ya dhahabu". Kuanzia hapa mto ni mpaka kati ya Uthai na Laos. Hapa unaitwa "Maè Nam Khong" katika nchi zote mbili. Kuanzia mji wa Luang Prabang unatumika kwa usafiri wa maboti na meli ndogo. Baada ya kupita mji Vientiane Mekong iko ndani ya eneo la Laos kwa kilomita chache. Kabla ya kuingia Kambodia mto unapita maporomoko ya Khone yanayozuia usafiri kwa meli kati sehemu za juu na chini za mto.

Nchini Kambodia Mekong inapita kwenye mji mkuu Pnomh Penh. Baadaye inajigawa katika mikono miwili: Mekong yenyewe na mkono unaoitwa Bassac.

Delta ya Mekong inaendelea katika kusini ya Vietnam hadi kuishia baharini.

Miji mikubwa mtoni

hariri
 
Nchi za beseni ya Mekong
(beseni: mstari uliovunjika)