Mpiji ni mto cha mkoa wa Pwani na mkoa wa Dar es Salaam na ni mpaka baina ya mikoa hiyo ya Tanzania.

Chanzo chake kipo karibu na Maneromango. Mpiji inapita Kibaha na Kerege inapoelekea kuishia katika Bahari Hindi.

Mwendo wake una urefu wa km 12.7. Unakusanya maji katika beseni la kilomita za mraba 52.

Kama mto muhimu katika eneo lenye wakazi wengi, Mpiji imeathiriwa na uharibifu wa mazingira kutokana na kuingizwa kwa maji machafu kutoka karakana na viwanda na matumizi ya maji mengi kwa umwagiliaji na madhumuni mengine.[1]. Uchimbaji wa mchanga kwa ajili ya ujenzi wa nyumba unaathiri pia ekolojia ya mto[2].

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Dar rivers in danger of drying up, gazeti la The Citizen, 28.05.2017
  2. Kilio cha wakazi wa bunju na mbweni juu ya uharibifu wa mazingira bonde la mto Mpiji , blogu ya Issa Mchuzi, Mei 2016

Viungo vya nje hariri