Mto Verlorevlei unapatikana katika jimbo la Rasi Magharibi, Afrika Kusini. Lango la mto huo linapatikana katika ghuba ya Elands.

Miongoni mwa matawimto ya mto huo ni mto Hol, mto Kruismans na mto Krom Antonies.

Mto huu ndio makazi pekee inayotambulika kwa viumbe vilivyo hatarini.[1]

Ziwa lenye asili ya tope lililopo takribani kilometa 30 kutoka kaskazini magharibi mwa Redelinghuys ndilo chanzo cha mto huu. Wakati wa majira ya baridi, maji hufichama chini ya nyasi za kijani na wakati wa kiangazi ziwa huwa linakauka.

Aina 500 za ndege wamekwisha onekana katika ziwa hilo. Ikiwa Ziwa Verlorevlei ni moja kati ya maziwa machache ya maji safi, pia ni eneo muhimu katika uzalishaji na ufugaji wa flamingo, mwari pamoja na aina mbalimbali za samaki na ndege wengine. Jamii nyingi za mimea hupatikana pia katika ziwa hilo.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Chakona, Albert; Swartz, Ernst R.; Skelton, Paul H. (11 November 2014). "A new species of redfin (Teleostei, Cyprinidae, Pseudobarbus) from the Verlorenvlei River system, South Africa". ZooKeys (Pensoft) 453 (453): 121–137. PMC 4258629. doi:10.3897/zookeys.453.8072. Iliwekwa mnamo 4 December 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Verlorevlei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.