Bupe kibona
Mia Krisna Pratiwi
haririMia Krisna Pratiwi ni raia wa indonesia, mhandisi na mwanamazingira. alitajwa kwenye orodha ya wanawake mia moja wa BBC mwaka 2021[1]
Pratiwi alisoma kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Bandung na anafanya kazi katika Shirika la Mazingira jijini Denpasar. Pratiwi aliendeleza programu ya kompyuta ya kuboresha ukusanyaji, usindikaji na kuchakata taka za mijini katika kisiwa cha Bali. programu hiyo ilisimamiwa na shirika lisilo la kiserekali linalojulikana kama Griya Luhu.[1][2]
Mnamo Oktoba 2021, Pratiwi alikuwa mmoja wa majaji wa Mashindano ya wajasiriamali Vijana.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "BBC 100 Women 2021: Who is on the list this year?" (kwa Kiingereza (Uingereza)). BBC News. 2021-12-07.
- ↑ RTV News, mhr. (2022-01-03). "Jagoan 2021 : Mia Krisna Pratiwi, Mengolah Sampah Jadi Rupiah" (kwa Kiindonesia). Iliwekwa mnamo 2022-02-21.
- ↑ Precious Island, mhr. (2021-11-16). "Global Youth Conference Mengumumkan Pemenang Sustainable Teenpreneur Competitions" (kwa Kiindonesia). Iliwekwa mnamo 2022-02-21.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Bupe kibona kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Marie Christina Kolo
haririMarie Christina Kolo(amezaliwa mwaka 1989) ni mwanaharakati na mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa, ecofeminist, na mjasiriamali kutoka Madagascar, ambaye ameongeza ufahamu wa kimataifa juu ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa huko Madagascar na kuomba mshikamano wa kimataifa katika kushughulikia athari zake.
Maisha
haririKolo alizaliwa mwaka 1989 na kulelewa uko Ambodirano.[1] Alipokua Mdogo, aliona athari za mazingira zinazosababishwa na viwanda vya nguo karibu na nyumba yao, na akatoa ombi la kukomesha uchafuzi. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Paris na akapata shahada ya uzamili katika Usimamizi wa Mradi na maendeleo ya jamii.[2]Alitunukiwa cheti na Chuo Kikuu cha Mandela Washington Fellowship mnamo mwaka 2017.
Kolo alijiunga kwenye maswala ya hali ya hewa mnamo 2015, akiwa kama mfanyakazi wa kujitolea katika shirika la Umoja wa Mataifa huko Androy. [3] Wakati huo, Kolo alishiriki kuanzisha Mtandao wa Hali ya Hewa ya Bahari ya Hindi kama jukwaa la majadiliano kwa vijana wanaofanya kazi kutoka Madagascar, Mauritius, Réunion, na Seychelles.[1][2][3][4] [1] Jukwaa hilo lilikua na watu 3000 waliohudhuria maandamano ya kwanza ya hali ya hewa ya Madagaska mnamo mwaka 2015.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Marie Christina Kolo: La lucha para que Madagascar sobreviva". Columna Digital (kwa Mexican Spanish). 2022-03-17. Iliwekwa mnamo 2022-03-22.
- ↑ 2.0 2.1 "Madagascar 2017 - UMaine Mandela Washington Fellowship - University of Maine". UMaine Mandela Washington Fellowship (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
- ↑ 3.0 3.1 "Portrait : Marie Christina Kolo, la révoltée de Madagascar". Vanity Fair (kwa Kifaransa). 2020-10-07. Iliwekwa mnamo 2022-03-22.
- ↑ "MARIE CHRISTINA KOLO". Emerging Valley (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Bupe kibona kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |