Shelisheli
Shelisheli pia Ushelisheli, kwa jina rasmi Jamhuri ya Shelisheli (kwa Kifaransa: République des Seychelles; kwa Krioli Repiblik Sesel), ni nchi ya funguvisiwa katika Bahari Hindi, mashariki kwa mwambao wa Afrika Mashariki na kaskazini kwa Madagaska. Nchi hiyo ya visiwa inajumuisha visiwa 155 (kulingana na Katiba). Mji mkuu wake na mji mkubwa zaidi, Victoria (Shelisheli), uko kilomita 1,500 (milia za baharini 800) mashariki ya bara la Afrika. Nchi za visiwa na maeneo ya jirani ni Komoro, Madagaska, Morisi, na idara za ng'ambo za Ufaransa za Mayotte na Réunion kusini; na funguvisiwa la Chagos upande wa mashariki. Shelisheli ni nchi iliyo ndogo zaidi barani Afrika pamoja na kuwa nchi ya Kiafrika iliyo na idadi ndogo zaidi ya watu, ikiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa 100,600 mwaka 2022
Jamuhuri ya Ushelisheli République des Seychelles (Kifaransa) Repiblik Sesel (Kimaori) | |
---|---|
Kaulimbiu: "Finis Coronat Opus" (Kilatini) "Mwisho hutunuku taji kazi" | |
Wimbo wa taifa: "Koste Seselwa" Join together all Seychellois | |
Mji mkuu na mkubwa | Victoria (Shelisheli) |
Lugha rasmi |
|
Kabila |
|
• Wavel Ramkalawan | Rais |
• Ahmed Afif | Makamu wa Rais |
Dominion (kujitawala) | |
Eneo | |
• Jumla | km2 268,680 km² (ya 75) |
• Maji (asilimia) | 2.1% |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2021 | 130,523 |
• Msongamano | 19.1/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ![]() |
• Kwa kila mtu | ![]() |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ![]() |
• Kwa kila mtu | ![]() |
HDI (2022) | 0.802 |
Gini (2019) | 32.1 |
Sarafu | Rupea ya Ushelisheli (SCR) |
Majira ya saa | UTC+04:00 (SCT) |
Msimbo wa simu | +248 |
Jina la kikoa | .nz |


Jiografia
haririShelisheli ina visiwa 115; 32 kati ya hivyo ni visiwa vikubwa kidogo vyenye milima, vingine ni vidogo na huitwa "Visiwa vya nje".
Kisiwa kikubwa zaidi ni Mahé na mji mkuu Victoria uko huko. Wakazi wengi huishi Mahe pamoja na visiwa vya karibu, hasa Praslin na La Digue.
Visiwa hivyo vina milima inayofikia hadi mita 900 juu ya UB. Mkubwa ni Morne Seychellois wenye mita 905 juu ya UB.
Hali ya hewa ni ya kitropiki ikiwa halijoto iko kati ya 24 °C na 30 °C. Kiasi cha mvua ni kati ya mm 2.880 huko Victoria na mm 3.550 mlimani.
Historia
haririHakuna hakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu.
Taarifa ya kwanza imepatikana kutoka kwa Wareno waliozunguka hapa kuanzia mwaka 1505.
Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa au kukusanya matunda bila ya kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.
Ndio Ufaransa uliojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wao wa siku zile Jean Moreau de Sechelles.
Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe.
Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Waingereza walivumilia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.
Kwanza Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius, lakini mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni mbali na Mauritius.
Mwaka 1970 Shelisheli walipata uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uingerezeza lakini mwaka 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja.
Tangu 1993 katiba ilisahihishwa tena ikiruhusu vyama vingi vya kisiasa.
Chama kilichopata kura nyingi ndicho SPPF (Seychelles People's Progressive Front).
Demografia
haririKabila
haririWakazi kwa jumla (93.2%) ni machotara wenye mchanganyiko wa damu ya Afrika bara, Ulaya na Asia. Licha ya hao kuna vikundi vidogo vya Wahindi (6%), Wazungu (5%) na Wachina (0.5%) halisi.
Lugha
haririLugha rasmi ni tatu: Kiingereza (5.1%), Kifaransa (0.7%) na Kiseselwa, aina ya Krioli ambayo imetokana na Kifaransa na ndiyo lugha ya kawaida (91%).
Dini
haririUpande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (76.2%), halafu Waprotestanti (13.0%), wengine wachache ni Wahindu (2.4%), Waislamu (1.6%) n.k.
Uchumi
haririUchumi wa Shelisheli unategemea zaidi utalii, uvuvi, na huduma za kifedha. Ikiwa na Pato la Taifa (GDP) la $2.08 bilioni (2022) na Pato la Taifa kwa kila mtu la $20,880, Shelisheli imeorodheshwa kama nchi yenye kipato cha juu na Benki ya Dunia na ndiyo nchi tajiri zaidi barani Afrika. Licha ya mafanikio yake ya kiuchumi, nchi inakabiliwa na changamoto kama ukosefu wa usawa wa mapato, utegemezi wa uagizaji bidhaa, na hatari za kiuchumi kutoka nje.[1]
Viashiria vya Kiuchumi
hariri- Pato la Taifa (Nominal, 2024): $2.085 bilioni
- Pato la Taifa kwa Kila Mtu (2024): $20,889
- Kiwango cha Ukuaji wa Pato la Taifa (2022): 8.2%
- Kiwango cha Mfumuko wa Bei (2022): 2.6%
- Kiwango cha Ukosefu wa Ajira (2021): 4.8%
- Deni ya Umma kwa Pato la Taifa (2022): 64.9%
Utalii
haririUtalii ndio sekta kubwa zaidi ya uchumi wa Shelisheli, ikichangia takriban 25% ya Pato la Taifa na kutoa ajira kwa zaidi ya 30% ya wafanyakazi moja kwa moja au kupitia sekta zinazohusiana. Kabla ya janga la COVID-19, Shelisheli ilipokea watalii 428,000 mwaka 2019, wengi wakitoka Ulaya. Sekta hii ilirejea kwa nguvu mwaka 2022, na zaidi ya watalii 330,000 waliwasili, wakileta mapato ya karibu $1 bilioni.
- Idadi ya Watalii (2019): 428,000
- Idadi ya Watalii (2022): 330,000
- Mchango wa Utalii kwa Pato la Taifa: ~25%
Uvuvi
haririShelisheli ina Eneo la Kiuchumi la Kipekee (EEZ) la kilomita za mraba milioni 1.3, jambo linalofanya uvuvi kuwa sekta muhimu. Uvuvi unachangia karibu 20% ya Pato la Taifa na hutoa ajira kwa zaidi ya watu 5,000. Uuzaji wa samaki nje ya nchi, hasa samaki wa jodari (tuna), unachangia zaidi ya 95% ya mapato ya mauzo ya nje, huku Umoja wa Ulaya ukiwa soko kuu.
- Mchango wa Uvuvi kwa Pato la Taifa: ~20%
- Mapato kutoka Uuzaji wa Samaki (2022): ~$450 milioni
- Ajira katika Sekta ya Uvuvi: ~5,000
Huduma za Kifedha
haririShelisheli ina sekta imara ya kifedha ya nje ya nchi (offshore finance), ikiwa na zaidi ya makampuni 200,000 ya biashara ya kimataifa yaliyosajiliwa. Sekta hii inachangia 10-15% ya Pato la Taifa na ni chanzo kikubwa cha mapato ya fedha za kigeni. Hata hivyo, Shelisheli imekuwa chini ya uangalizi wa kimataifa kuhusu uwazi wa kifedha na sheria za kupambana na utakatishaji fedha.
- Mchango kwa Pato la Taifa: 10-15%
- Makampuni ya Kifedha yaliyosajiliwa: ~200,000
Kilimo na Uzalishaji Viwandani
haririKilimo kinachangia chini ya 2% ya Pato la Taifa, kwani Shelisheli inategemea sana uagizaji wa chakula kutokana na ardhi ndogo inayofaa kwa kilimo. Mazao makuu ni nazi, vanilla, na mdalasini. Sekta ya viwanda, haswa usindikaji wa chakula (hususan makopo ya samaki), inachangia 5-8% ya Pato la Taifa.
- Mchango wa Kilimo kwa Pato la Taifa: <2%
- Mchango wa Uzalishaji Viwandani kwa Pato la Taifa: 5-8%
Biashara na Fedha za Kigeni
haririShelisheli inategemea sana uagizaji wa bidhaa, ambapo zaidi ya 70% ya Pato la Taifa linatokana na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje. Bidhaa kuu zinazoagizwa ni chakula, mashine, na bidhaa za mafuta, huku mauzo ya nje yakitawaliwa na samaki waliyochakatwa na huduma za utalii. Washirika wakuu wa biashara ni Umoja wa Ulaya, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), na India.
- Thamani ya Uagizaji (2022): ~$1.2 bilioni
- Thamani ya Uuzaji wa Bidhaa Nje (2022): ~$500 milioni
- Bidhaa Kuu ya Mauzo ya Nje: Samaki waliyochakatwa (95% ya mauzo)
Washirika Wakuu wa Biashara: Umoja wa Ulaya, UAE, India
Changamoto
haririShelisheli inakabiliwa na changamoto kadhaa za kiuchumi:
- 1. Deni ya Umma Kiasi Kikubwa: Ingawa deni limepungua kutoka zaidi ya 90% ya Pato la Taifa mwaka 2020 hadi 64.9% mwaka 2022, bado linabaki kuwa tatizo.
- 2. Utegemezi Mkubwa kwa Utalii: Ukuaji wa uchumi unategemea sana sekta ya utalii, ambayo ni nyeti kwa changamoto za kimataifa kama vile janga la COVID-19.
- 3. Hatari Zinazotokana na Mabadiliko ya Tabianchi: Kupanda kwa usawa wa bahari na uharibifu wa mazingira baharini kunaweza kuathiri sekta ya uvuvi na miundombinu ya utalii.
- 4. Ukosefu wa Usawa wa Mapato: Ingawa Shelisheli ina Pato la Taifa kwa kila mtu miongoni mwa ya juu zaidi barani Afrika, gharama ya maisha ni kubwa na inaathiri zaidi tabaka la chini la jamii.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ World bank. "Uchumi wa Shelisheli" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-23.
Viungo vya nje
hariri- Serikali
- State House, Office of the President of the Republic of Seychelles
- Central Bank of Seychelles, on-shore banking and insurance regulator
- Seychelles International Business Authority (SIBA) Ilihifadhiwa 3 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine., regulator of off-shore financial sector
- Seychelles Investment Bureau Ilihifadhiwa 30 Novemba 2018 kwenye Wayback Machine., government agency promoting investment in the Seychelles
- National Bureau of Statistics, government agency responsible for collecting, compiling, analysing and publishing statistical information
- Serikali ya Shelisheli mtandaoni
- US Department of State, Background Note: Seychelles
- Dini
- Taarifa za jumla
- Seychelles entry at The World Factbook
- Seychelles Ilihifadhiwa 25 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Shelisheli katika Open Directory Project
- Seychelles from BBC News
- Wikimedia Atlas of Seychelles
- Island Conservation Society, a non-profit nature conservation and educational non-governmental organisation
- Nature Seychelles, a scientific/environmental non-governmental nature protection association
- The Seychelles Nation, the largest circulation local daily newspaper
- Seychelles Bird Records Committee
- Seychelles.travel Ilihifadhiwa 4 Agosti 2021 kwenye Wayback Machine., Government tourism portal
- Air Seychelles, Seychelles national airline
- ADST interview with U.S. Ambassador to the Seychelles David Fischer
- Private website with tips and images
Shelisheli travel guide kutoka Wikisafiri
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Shelisheli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |