Deborah John Ngira
Mimi naitwa Deborah John Ngira ni mtanzania nilizaliwa tarehe 25 mwezi wa 1 mwaka 2002 nina miaka 20. Baba yangu anaitwa John Ngira na mama anaitwa Juliana John ndio waliyo fanikiwa kunileta duniani nawapenda sana pia sipo mwenyewe kwenye familia yangu tupo watoto wa nne wa kwanza ni dada yangu anaitwa Hefsiba wa pili ni mimi Deborah wa tatu anaitwa Doreen na wa mwisho ni mdogo wetu wa kiume pekee anaitwa Harryson hii ndio familia yangu ambayo ipo kwa mgawanyo wa herufi za kwanza za majina kufanana ambayo, J ya mama na baba,H ya mzaliawa wa kwanza na wa mwisho na nyingine ni D ni ya wazaliwa wa katikati me na familiya yangu tulifurahi pale wazazi wetu walikuja kutuambia kuhusu hizi herufi na tulipenda hiki kitu. Mimi ni mchagga ila mzaliwa wa Arusha pia mimi na familia yangu tunampenda Mungu na kumshukuru apa alipotufikisha. Kuhusu mimi nilisoma shule ya msingi Inayoitwa Haradali pre and primary school iliyopo arusha ndio nilipochukulia elimu yangu ya msingi mpka mwaka 2015 nikaitimu darasa la saba.Nikaenda kuchukulia elimu yangu ya sekondari vunjo secondary high school iliyopo moshi ila siku fanikiwa kuhitimu pale nilihama na kwenda kusoma shule nyingine kuanzia kidato cha pili inayoitwa Ngarenanyuki secondary and high school iliyopo arusha apo ndipo nikaitimu kidato cha nne mwaka 2019. Nilipo maliza kidato cha nne nilipangiwa chuo cha elimu ya biashara mwanza (CBE) na nikachukulia kozi ya procurement and supply management (ugavi) nilisoma mwaka mmoja mwanza na nikaja kuhami dodoma na bado na soma ila lengo langu lilikuwa kusomea pharmacy ya madical nilikuwa napenda kuja kufanya kazi zakutengeneza madawa sana ila ndoto yangu bado naamini nitakuja kuikamilisha siku moja. Napenda siku moja nije kuishi jamaica nilipenda kuwaza ivyi kwa pale ambopo nilikuja kusoma stori kuhusu jamaika na kuona maisha wanayoishi na nilitokea kupenda sana na nilikuwa na penda nyimbo za lucky dube na bob marley na nikapata jina watu wakiniita mjamaica lady na kuanzia apo nikajikubali na kuishi uko.kuhusu kuwa mwana wikimedia nilianzi arusha tukio la women’right ndipo nilienda nakupenda wanachofanya kusaidia jamii siyo tu kwa wale wenyeelimu ya juu kusoma kingereza ila ata ngazi ambazo hazijui kingereza, unapata makala imetafsiriwa kwa lugha ambayo unahielewa, na kuandika pia stori ambazo watu wanatakujua kuanzia apo mpaka sasa napenda hili shirika . Nafanya kazi pia na kampuni ya Goodlife property inayo husika na huuzaji wa viwanja mikoani kama Dodoma,Dar es salaam,Mwanza na Arusha. Ninacho muomba Mungu ni kwamba watoto wangu wasije kuishi maisha niliyo lelewa mimi bali waishi maisha mara mbili niliyo yaishi ndio msemo ninaosimama nao nanitautimiza . Msemo ninao hupenda kwenye maisha ya sasa ili hufikie lengi lako bila kukatishwa tamaa na wanaokuzunguka “fanya kile unachopenda, penda unachofanya” hiki ndicho kuhusu mimi kwa ufupi.