Mtunguru (mmea)
(Elekezwa kutoka Mtungulu)
Mtunguru | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mtunguru wa Zambesi (Aframomum zambesiacum)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 50 |
Mitunguru, mitungulu, mitunguu au miiliki mwitu ni mimea ya kudumu ya jenasi Aframomum katika familia Zingiberaceae (familia ya mtangawizi). Mbegu za spishi nyingi hutumika kama kiungo ambacho ladha yake inafanana na pilipili manga au iliki.
Mimea hiyo hutokea Afrika kusini mwa Sahara. Ina mashinaukoka ambayo hutoa mashina marefu ya hadi m 2 au zaidi kutoka kwa mafundo yao. Mashina hayo yanabeba majani yasiyoelekeana hadi sm 30 kwa urefu. Maua hukua kwa vishada kwenye mashina mafupi yanayotoka moja kwa moja kutoka kwa shinaukoka.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Aframomum albiflorum, Mtunguru Maua-meupe
- Aframomum amaniensis, Mtunguru wa Usambara
- Aframomum angustifolium, Mtunguru Majani-membamba
- Aframomum corrorima, Mtunguru wa Kawaida au mwiliki bandia
- Aframomum mala
- Aframomum melegueta - inakuzwa nchini Ethiopia
- Aframomum orientale
- Aframomum spiroligulatum
- Aframomum uniflorum
- Aframomum verrucosum
- Aframomum zambesiacum, Mtunguru wa Zambesi au nangawo
Picha
hariri-
Matunda ya mtunguru majani-membamba
-
Matunda ya mtunguru wa Zambesi
-
Iliki bandia