Mukund Varadarajan
Meja Mukund Varadarajan (12 Aprili 1983 - 25 Aprili 2014) alikuwa afisa wa Jeshi la India na mpokeaji wa tuzo ya Ashoka Chakra. Afisa Mukund, aliyeteuliwa katika Kikosi cha Rajput cha Jeshi la India, alitunukiwa tuzo ya Ashok Chakra baada ya kifo chake kwa ajili ya matendo yake wakati wa operesheni ya kukabiliana na ugaidi, alipokuwa akihudumu katika kikosi cha 44 cha Rashtriya Rifles huko Jammu na Kashmir. Filamu yake ya wasifu kwa lugha ya Kitamil, Amaran, ilitolewa wakati wa Sikukuu ya Diwali, tarehe 31 Oktoba 2024.
Maisha ya Awali na Elimu
haririMukund Varadarajan alizaliwa katika Kijiji cha Paruthipattu, Avadi, Chennai, Tamil Nadu, India,[1] katika familia ya R Varadarajan na Geetha Varadarajan inayozungumza lugha ya Kitamil.[2] Baadaye, yeye na familia yake walihamia Tambaram baada ya babake kupata kazi katika Benki ya Sekta ya Umma.[1] Pia Babu yake Raghavachari na wajomba zake wawili walihudumu katika jeshi, jambo ambalo lilipa motisha ya kujiunga na Jeshi.[2] [3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "அமரன்: மேஜர் முகுந்த் வரதராஜன் யார்? அவரது கடைசி தருணம் எப்படி இருந்தது?". BBC News தமிழ் (kwa Kitamili). 2024-10-30. Iliwekwa mnamo 2024-11-03.
- ↑ 2.0 2.1 "Tambaram mourns a braveheart", 27 April 2014.
- ↑ "Major Worked at BPO Before Realising Childhood Dream", 27 April 2014. Retrieved on 2024-12-08. Archived from the original on 2014-04-28.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mukund Varadarajan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |