Kuua kwa kukusudia

(Elekezwa kutoka Murder)

Kuua kwa kukusudia (kwa Kiingereza: murder) ni kosa la jinai kadiri ya sheria ambapo mtu mmoja anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa makusudi na kwa nia mbaya.

Polisi kwenye mahali pa uuaji kwa kusudi mjini Rio de Janeiro, Brazil

Katika sheria za Tanzania

Sheria ya Tanzania inafafanulia: "Mtu yeyote ambaye, kwa dhamira ya uovu, anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa kitendo kisicho halali au kuacha kutenda ana hatia ya kuua kwa kukusudia."[1]

Adhabu ya kuua kwa kukusudia ni adhabu ya kifo[2], ingawa adhabu hiyo haijatekelezwa tena Tanzania tangu mwaka 1994[3], nchini Kenya tangu 1987, Uganda tangu 2005 https://www.pgaction.org/ilhr/adp/uga.html[4].

Adhabu yake

Idadi ya nchi zilizofuta adhabu ya kifo inazidi kuongezeka[5].

Katika sheria za kisasa uuaji wa makusudi hutazamwa kama jinai dhidi ya jamii unaopaswa kuadhibiwa na dola. Katika mifumo ya sheria ya kimapokeo ulitazamwa mara nyingi kama jambo la binafsi, pia kwa kutotofautisha kati ya kuua kwa kusudi na bila kusudi; hapo ukoo wa aliyeuawa alikuwa na haki ya kulipiza kisasi kwa kumwua muuaji au ndugu wake. Ili kupakana marudio ya kisasi mifumo mingi ya kimapokeo ilijua pia malipo ya fidia.

Mfumo wa fidia unapatikana katika nchi kadhaa (mfano Iran, Saudia, Pakistan) zinazofuata sharia ya Kiislamu ambako ni juu ya familia ya aliyeuawa kuamua kuhusu fidia au utekelezaji wa adhabu ya kifo.

Marejeo

  1. Kiingereza: "Any person who, with malice aforethought, causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilty of murder." Tanzania Proncipal Legislation, Chapter 16, The Penal Code, Chapter XX, Muder and manslaughter, ss. 196. online hapa
  2. Ss 197.
  3. Tanzania and the Death Penalty, tovuti ya PGA - Parlamentarians for Global Action, iliangaliwa February 2021
  4. Uganda and the Death Penalty, tovuti ya PGA - Parlamentarians for Global Action, iliangaliwa February 2021
  5. [https://achpr.org/public/Document/file/English/study_question_deathpenalty_africa_2012_eng.pdf Study on the question of the Death Penalty in Africa] Ilihifadhiwa 23 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine., African Commission on Human and Peoples’ Rights , Banjul, The Gambia

Viungo vya Nje

 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuua kwa kukusudia kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.