Adhabu ya kifo ni mauaji ya mwanadamu yanayotekelezwa na serikali baada ya mahakama kutoa hukumu ya mauti kulingana na sheria za nchi.

Adhabu ya kifo duniani. Buluu: hakuna,
Kijani: Adhabu ya kifo wakati wa vita pekee; kichungwa: kuna adhabu ya kifo lakini haikutekelezwa katika miaka 10 iliyopita
Nyekundu:Adhabu ya kifo hutolewa

Kwa kawaida adhabu hiyo inatolewa kwa jinai nzito sana.

Sababu za kumhukumu mtu afe

hariri
 
Kitabu cha Cesare Beccaria, Dei delitti e delle pene

Zamani ilikuwa adhabu ya kawaida katika nchi nyingi kwa wauaji hasa, lakini pia kwa makosa kama unajisi, biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi.

Kihistoria hata aina za upinzani dhidi ya mtawala wa nchi ziliadhibiwa kwa adhabu ya mauti: mara nyingi iliitwa kusaliti taifa au kuhatarisha usalama wa nchi.

Kuna pia nchi ambako kuondoka katika dini rasmi kuliadhibiwa hivyo.

Kwa jumla kuna hasa sababu nne zinazotajwa kwa ajili ya adhabu ya kifo:

  1. adhabu hii ni dia inayotakiwa kwa jinai nzito. Mtu aliyeua hastahili kuishi tena. Haki inadai ya kwamba adhabu ilingane na tendo.
  2. Adhabu ya kifo inaondoa wakosaji wa hatari katika jamii. Hawawezi kutoroka au kuachishwa jela na kuleta hatari ya kwamba atarudia matendo yale.
  3. Watu wengine wanaotafakari kutenda maovu yale wataogopa kufanya hivyo kwa hofu ya adhabu ya kifo, hivyo hofu hii inaongeza kiwango cha usalama katika jamii.
  4. Heri kumwua mkosaji aliyeua kuliko kumfunga ndani kwa maisha yake kwa sababu hii:
    • inaleta gharama kubwa kwa jamii
    • ni adhabu ya kinyama zaidi kuliko kumwua mkosaji

Upinzani

hariri

Katika karne ya 20 upinzani dhidi ya adhabu hii ilipata nguvu, na nchi nyingi zimefuta adhabu ya kifo. Katika nchi nyingine adhabu iko bado kisheria, lakini haikutekelezwa tena tangu miaka mingi kwa mfano katika Kenya na Tanzania.

Sababu za upinzani ni hasa kama zifuatazo:

  1. wengi hudai ya kwamba adhabu ya kifo hailingani na utu. Katika hoja hii kumwua mtu ni kinyama na hata kama mkosaji alimwua mtu mwingine na kutenda unyama huu si sababu nzuri kwa umma au jamii kushuka chini kwenye ngazi hiyohiyo na kumtendea mksosaji jinsi alivyotenda mwenyewe.
  2. Adhabu ya kifo ni adhabu ambayo haiwezi kurekebishwa. Lakini kila mahakama inaweza kukosa na kuna mifano mingi ya kwamba mahakama ilikosa na kumhukumu mtu kuwa alihusika na jinai lakini baadaye ilionekana si yeye. Kama amefungwa jela anaweza kuachishwa na kurudishiwa uhuru. Kama ameshauawa hakuna njia ya kumrudishia uhai.
  3. Hakuna uthibitisho wa kwamba adhabu ya kifo inasaidia kupunguza jinai katika jamii.

Nchi zilizotekeleza hukuma ya kifo mara nyingi

hariri

Mwaka 2005 watu waliuawa na serikali baada ya hukumiwa katika nchi zifuatazo:

  1. China (angalau watu 1,770)
  2. Uajemi (angalau 94)
  3. Saudi Arabia (angalau 86)
  4. Marekani (60)
  5. Pakistan (31)
  6. Yemen (24)
  7. Vietnam (21)
  8. Jordan (11)
  9. Mongolia (8)
  10. Singapur (6)
  11. Uturuki (3)
  12. Ufaransa (1)

Namna za kutekeleza adhabu ya mauti

hariri
  • Kupiga risasi
  • Sindano ya sumu
  • Kunyonga
  • Kukata kichwa
  • Kiti cha umeme
  • Kurusha mawe

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons


Wanaopinga adhabu ya kifo

hariri

Wanaotetea adhabu ya kifo

hariri

Mafundisho ya kidini

hariri