Kwa maana nyingine za jina hilo, tazama Muungano

Muungano ni kata ya Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania, yenye postikodi namba 57441.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,492 waishio humo[1].

Kata ya Muungano inaundwa na vijiji vitatu vya Kindimba Chini, Kimara na Kizota. Kijiji cha Kindimba Chini ndiyo makao makuu ya kata ya Muungano.

Kata ya Muungano ina shule za msingi nne. Shule ya Msingi Kindimba Chini iliyopo kijiji cha Kindimba Chini, Shule ya Msingi Kizota iliyopo kijiji cha Kizota, Shule ya Msingi Kimara na Shule ya Msingi Mapendano zilizopo kwenye kijiji cha Kimara. Kuna mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Upendo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Januari mwaka 2024 kwenye kijiji cha Kindimba Chini.

Wakazi wanapata huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Kindimba Chini.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania  

Amani Makoro | Kambarage | Kigonsera | Kihangi Mahuka | Kipapa | Kipololo | Kitumbalomo | Kitura | Langiro | Linda | Litembo | Litumbandyosi | Lukarasi | Maguu | Mapera | Matiri | Mbuji | Mhongozi | Mikalanga | Mkako | Mkumbi | Mpapa | Muungano | Namswea | Ngima | Nyoni | Ruanda | Ukata | Wukiro


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Muungano (Mbinga) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.