Mkoa wa Ruvuma


Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania.

Mkoa wa Ruvuma
Mahali paMkoa wa Ruvuma
Mahali pa Mkoa wa Ruvuma katika Tanzania
Majiranukta: 11°0′S 36°0′E / 11.000°S 36.000°E / -11.000; 36.000
Nchi Tanzania
Wilaya 6
Mji mkuu Songea
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Christine G. Ishengoma
Eneo
 - Jumla 63,498 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 1,848,794
Tovuti:  http://www.ruvuma.go.tz/

Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki.

Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.

WilayaEdit

Ndani ya mkoa huu kuna wilaya sita ambazo ni (idadi ya wakazi katika mabano):

WakaziEdit

Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794 (sensa ya mwaka 2022).

Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena na Wandengereko.

Karibu na Songea iko monasteri kubwa ya Peramiho ya watawa Wabenedikto na nyingine iko Hanga.

ElimuEdit

Elimu bado inahitajika, hasa kwa maeneo ya vijijini, maana watu wengi katika mkoa huu hawajaelimika hivyo huleta changamoto katika maendeleo maana taifa huhitaji watu ambao ni wasomi.

MiundombinuEdit

Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda [[Lindi] ni kiwango cha lami kuanzia Songea mjini kupitia Wilaya za Namtumbo, Tunduru, Nanyumbu, Masasi, Mnazimmoja-Lindi, hadi Dar es Salaam.

Majimbo ya bungeEdit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit