Kihangi Mahuka
Kihangi Mahuka ni kata ya Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania, yenye postikodi namba 57413.
Kata ya Kihangi Mahuka | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Ruvuma |
Wilaya | Mbinga |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 7,695 |
Kata hiyo imeundwa na vijiji vinne ambavyo ni: Kihangi Mahuka, Lipumba, Lihutu na Mahumbato (Nswika). Inapatikana mashariki ya wilaya ya Mbinga ikipitiwa na barabara kuu ya Mbamba Bay - Mtwara.
Jina limetokana na mlima Kihangi uliopo eneo hilo. Mahuka ni neno la lugha ya wenyeji ambao walikuwa wakiishi hapo.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 7,695 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,832 kabla ya kumegwa na kuzaa kata ya Lukarasi.[2]
Kati ya makabila yanayopatikana Kihangi Mahuka, kubwa ni la Wamatengo ambao ndi0 wazawa, pia kuna Wangoni, Wabena na Wahehe wachache.
Shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo: Wamatengo hao ni mahiri na wabobezi katika kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi, maharagwe, mbogamboga na matunda, ndizi (matoki), miwa, magimbi, viazi, ngano, ulezi na alizeti; vilevile mazao ya biashara hasa kahawa ambayo Kihangi Mahuka ni kwao na kwa kiasi kikubwa pia mitiulaya na tumbaku kidogo sana.
Kihangi Mahuka ina huduma za kijamii zikiwemo zahanati, shule za msingi na sekondari, maji safi, umeme na huduma za kiroho[3].
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Sensa ya 2012, Ruvuma - Mbinga District Council
- ↑ "Gmail". accounts.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
Kata za Wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania | ||
---|---|---|
Amani Makoro | Kambarage | Kigonsera | Kihangi Mahuka | Kipapa | Kipololo | Kitumbalomo | Kitura | Langiro | Linda | Litembo | Litumbandyosi | Lukarasi | Maguu | Mapera | Matiri | Mbuji | Mhongozi | Mikalanga | Mkako | Mkumbi | Mpapa | Muungano | Namswea | Ngima | Nyoni | Ruanda | Ukata | Wukiro |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kihangi Mahuka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |