Muwati
(Acacia spp.)
Muwati wa Madagaska
Muwati wa Madagaska
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Mimosoideae (Mimea inayofanana na kifauwongo)
Jenasi: Acacia (Miwati)
Mill., 1754
Spishi: Angalia katiba.

Miwati ni miti ya jenasi Acacia katika familia Fabaceae iliyo na majani yenye sehemu nyingi, lakini vikonyo vya majani vya spishi nyingi vimekuwa vipana na vimebadili majani menyewe. Zamani jenasi hii ilikuwa na spishi takriban 1300 lakini wanasayansi wameigawanya kwenye jenasi tano sasa: Acacia, Vachellia, Senegalia, Acaciella na Mariosousa[1]. Spishi za Acacia zinatofautiana na zile za jenasi Vachellia, Senegalia na Acaciella kwa ukosa wa miiba (ghairi ya muwati kangaruu). Hazina mastipula (majani mawili madogo chini ya jani kuu) kama spishi za Mariosousa. Kwa asili miti hii inatokea Australia lakini imewasilishwa katika mabara mengine.

"Majani" (vikonyo) ya muwati wa Madagaska

Spishi ya Afrika (Madagaska na kisiwa cha Reunion)Edit

Spishi zilizowasilishwa katika AfrikaEdit

PichaEdit

MarejeoEdit

  1. The Acacia Debate. Science In Public (2011). Iliwekwa mnamo 2011-08-03.