Muyaka bin Hajji
Muyaka bin Hajji (Mombasa, karne ya 18 - Mombasa, karne ya 19) alikuwa mshairi na mwandishi katika usultani wa Mombasa. Aliandika ushairi na hadithi zake kwa Kiswahili.
Muyaka Bin Hajji | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Muyaka Bin Hajji |
Alizaliwa | Karne ya 18 |
Alikufa | Karne ya 19 |
Nchi | Kenya, Mombasa |
Kazi yake | Mwandishi |
Alijulikana kuandika mashairi mengi kama Ngome, Kwa heri mwana, Kitandi au Ghazali.
Maisha yake
haririAliandikia vitabu vyake kwa sultani wa Mombasa. Jina lake (-yaka) linaonyesha alikuwa Mwafrika, tena wa Kibantu.
Mashairi yake
hariri- Ngome
- Kwa heri mwana
- Kitandi
- Ghazali
- Mashairi ya Hatari
- Mbwene
- 'Kajipaka 'tama
- Ahadi
- Wale
Mistari ya Ngome
haririNgome ni ngome ya mawe
Nafusi la kufusiza.
Ngome ni ya matumbawe
Na boriti kuikiza.
Ngome wetwapo sikawe
Enda hima na kufuza.
Ngome imetuumiza
Naswi tu mumo ngomeni.
Marejeo
hariri- Knappert, J. (1982). Four Centuries of Swahili Verse.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muyaka bin Hajji kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |