Mwatuko wa nyuklia

(Elekezwa kutoka Mwatuko nyuklia)

Mwatuko nyuklia (pia mgawanyo nyuklia)[1] kwa (Kiingereza nuclear fission) ni mchakato ndani ya atomu ambapo kiini cha atomu kinagawiwa kuwa vipande vidogo zaidi. Mchakato huo unaachisha nishati nyingi ukitumiwa katika tanuri nyuklia na pia katika mlipuko wa silaha ya nyuklia.

Mwatuko nyuklia: Atomu ya 235Urani inagongwa na nyutroni, inabadilishwa kuwa 236Urani ambayo si thabiti, inapasuka kwa atomi mbili za Bari na Kriptoni na kuachisha nishati pamoja na nyutroni.
Mfano wa mwatuko nyuklia: Atomu inagongwa na nyutroni; kiini kinapasuka na nyutroni za ziada pamoja na nishati hutoka

Mwatuko nyuklia hutokea ama kama unururifu (kwa Kiingereza radioactivity) au kama mmenyuko nyuklia (nuclear reaction).

Mwatuko huo unatokea tu kwenye atomu nzito sana, yaani zenye kiini cha atomu kikubwa. Ulitambuliwa mara ya kwanza kwenye atomu za urani.

Mwatuko nyuklia hutumiwa kwa teknolojia. Pale ambapo mchakato unaendeshwa polepole, kama katika tanuri nyuklia, nishati inayotoka hutumiwa kwa kutengeneza umeme. Pale ambapo mchakato unaongozwa kutokea kwa ghafla matumizi yake ni bomu la nyuklia.

Kiasi cha nishati kinachopatikana kwa njia ya mwatuko nyuklia kinazidi sana kile kinachopatikana kwa njia ya fueli za kikemia kama vile mafuta au gesi. Kwa hiyo ni chanzo cha nishati chenye uwezo mkubwa sana. Lakini kwa upande mwingine mabaki ya mchakato wa mwatuko nyuklia ni nururifu sana, hivyo kama sumu kushinda elementi kama urani zinazotumiwa kuanzisha mchakato huu na zinaendelea kuwa vile kwa miaka elfu hadi lakhi kadhaa. Wasiwasi kuhusu takataka nyuklia pamoja na uwezo mkubwa wa uharibifu wa silaha za kinyuklia zilisababisha upinzani na kuwa msingi wa majadiliano yanayoendelea katika nchi nyingi kuhusu swali kama ni vema kutumia nishati nyuklia au la.

Marejeo

hariri
  1. "Mwatuko nyuklia" ni pendekezo la KAST 1995 kwa ajili ya "nuclear fission", mgawanyo ni lugha ya TUKI-ESD
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwatuko wa nyuklia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.