Mýa

(Elekezwa kutoka Mya)

Mýa Marie Harrison (amezaliwa Washington, D.C., 10 Oktoba 1979) ni mwimbaji muziki wa R&B, mtunzi wa nyimbo, menguaji, mtayarishaji wa rekodi, na mwanamitindo kutoka Marekani.

Mýa
Mýa attending the Susan G. Komen's 8th Annual Fashion For The Cure event in Hollywood, CA in Septemba 2009.
Mýa attending the Susan G. Komen's 8th Annual Fashion For The Cure event in Hollywood, CA in Septemba 2009.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Mýa Marie Harrison
Amezaliwa 10 Oktoba 1979 (1979-10-10) (umri 45)
Washington, D.C., Marekani
Aina ya muziki R&B, soul, hip hop, urban
Kazi yake Mwimbaji-Mtunzi, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji, mnenguaji, mwanakoreografia
Ala Sauti, violin
Aina ya sauti Mezzo-soprano
Miaka ya kazi 1998–hadi sasa
Studio Interscope, Motown, Manhattan
Ame/Wameshirikiana na Pink, Dru Hill, Sisqó, Lil' Kim , Christina Aguilera, Z-RO, na Missy Elliott

Albamu yake ya kwanza iliitwa jina sawa na lake. Ilitolewa mnamo mwezi wa Aprili 1998 kupitia Interscope Records, na kuuza zaidi ya nakala milioni mbili nchini Marekani, na kupelekea kupata dhahabu kwa single ya "It's All About Me" akishirikiana na Sisqo.[1]

Albamu yake ya pili, yenye mauzo ya platinamu Fear of Flying, ilitolewa mnamo 2000 na kupata mafanikio kadha wa kadha nchini Marekani na pande zingine za dunia, kwa single ya "Case of the Ex" ikawa kibao kikali na kilichovuma zaidi cha Mýa, kwa kufikia nafasi ya kwanza kwenye Australian Singles Chart. Baada ya mwaka, Harrison amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Grammy Award kwa kibao kikali cha "Lady Marmalade", toleo la marudio ambalo amefanya na Christina Aguilera, Lil' Kim, na Pink kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Moulin Rouge! (2001).

Albamu yake ya tatu, Moodring, ilitolewa mnamo mwezi wa Julai 2003 nchini Marekani na kutunukiwa Dhahabu na RIAA. Kwa kufuatia kubadili-badili studio kadhaa, ilipelekea kuchelewesha kutolewa kwa albamu ya nne ya Mýa, Liberation (2007), ilitolewa kwa mtindo wa upakuzi kupitia intaneti huko nchini Japani pekee na kumfanya atoe 2008 Japan-albamu babkuwa ya Sugar & Spice.

Kuongoza ujuzi wake katika uigizaji na kazi za uungaji mkono bidhaa, Harrison ameweza kujiingiza kwenye utangazaji wa mabishara na makapuni kama vile Coca-Cola, Gap, Iceberg, Tommy Hilfiger, na Motorola na amepta kuwa na uhusika mfupi kwenye filamu kama vile Dirty Dancing: Havana Nights (2004), Shall We Dance? (2004), na Cursed (2005). Mnamo mwaka wa 2002, amecheza kwenye filamu ya Chicago ambayo ni tengenezo la pili la filamu ya mwaka wa 1975 ya Broadway-muziki Chicago, ambayo amejishindia tuzo la Screen Actors Guild Award.[2]

Harrison alikuwa mshiriki kwenue msimu wa tisa wa Dancing with the Stars.[3] Billboard wamempa Mýa nafasi ya 97 katika orodha Wasanii Hot 100 wa miaka ya 2000.[4]

Diskografia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Mýa - Timeline". Rock on the Net. Iliwekwa mnamo 2009-04-10.
  2. "Awards for Mya". IMDb. Iliwekwa mnamo 2009-04-11. {{cite web}}: line feed character in |title= at position 11 (help)
  3. Joyce Eng. "Dancing with the Stars 2009 Season 9 Cast Revealed!", TVGuide.com, 2009-08-17. Retrieved on 2009-08-17. 
  4. http://www.billboard.com/#/charts-decade-end/hot-100-artists?year=2009&begin=91&order=position

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: