Narriman Jiddawi ni mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, idara ya sayansi ya baharini.[1] Ni mtaalamu katika kufundisha na utafiti kwenye sayansi ya bahari. Kazi zake kwenye sayansi ya bahari zinajikita zaidi juu ya uchambuzi wa kijaamii na kiuchumi,uundaji wa sera, uwezeshaji wa wadau ili kukuza uhifadhi wa bahari.[2]

Narriman alipata shahada ya awali katika zoolojia/botania katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia shahada ya uzamili kwenye biolojia ya uvuvi na usimamizi kutoka University of North Wales shahada ya uzamivu kwenye biolojia ya baharini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[3]

Narriman amekuwa mwanasayansi mwandamizi katika sayansi ya bahari, ambapo amechapisha makala mbalimbali kuhusu kilimo cha baharini, uwezeshaji wa wanawake katika ukanda wa pwani na usimamizi wa viumbe vilivyo hatarini kutoweka wakiwemo pomboo na kasa[4][5]. Pia anasemwa kufanya kazi kwenye mradi wa mabadiliko ya tabia nchi na uchumi wa buluu[6]

Akiwa mwanachama wa Pew cheritable Trusts alijikita zaidi katika kukuza hifadhi ya bahari kwa kuendeleza hesabu za mifumo ikolojia ya baharini kwa kuzingatia mfano wa Zanzibar, na kupitia hili aliweza kuwapa watunga sera viashiria vya kiuchumi na uchanganuzi kutoka kwa hesabu ili kusaidia sera muhimu kwa uhifadhi wa bahari.[7]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Narriman Jidawi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.