Nasir Jones (amezaliwa 14 Septemba 1973) ni mwanamuziki wa rap na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake kisanii kama Nas. Zamani alikuwa akijiita Nasty Nas. Nas ni mtoto wa mwanamuziki wa jazz wa zamani Mzee Olu Dara. Alizaliwa na kukulia katika nyumba za miradi za mjini (nyumba za watu wenye kipato cha chini) Queensbridge, New York.

Nas
Nas, akiwa mjini Paris, mnamo 2014
Nas, akiwa mjini Paris, mnamo 2014
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Nasir Jones
Pia anajulikana kama Nasty Nas
Amezaliwa 14 Septemba 1973 (1973-09-14) (umri 50)
Asili yake Queensbridge, New York City, New York, Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapa
Mtunzi wa Nyimbo
Mtayarishaji wa rekodi
Mwigizaji
Ala Sauti
Studio Ill Will/Columbia
The Jones Experience/Def Jam
Ame/Wameshirikiana na Weside Connection
AZ
Bravehearts
Nashawn
Kelis
Foxy Brown
Chrisette Michele
Nature
Jay-Z
Kanye West
The Game
Rakim
Busta Rhymes
Salaam Remi
L.E.S.
Large Professor,
DJ Premier
Dr. Dre
Lauryn Hill
Tovuti Nas.Defjam.com

Nas alisaini mkataba na studio ya Columbia Records mnamo mwaka wa 1994, na kutoa albamu yake ya kwanza ya Illmatic. Albamu ya Illmatic ilipata kuwa bora na kufahamika zaidi na mauzo bora.

Baadaye albamu kadhaa za Nas zilifuata. Albamu hizo ni pamoja na It Was Written ya 1996, I Am... and Nastradamus ya 1999, na Stillmatic ya 2001. Nas alikuwa mmoja kati ya wanakundi la muziki wa rap na hip hop - The Firm, ambalo limejumuisha wasanii wengine kama vile AZ, Foxy Brown, na Nature. Ingawa kundi halikufanya kazi nyingi lilifanikiwa kutoa albamu moja ya pamoja.

Kuanzia mwaka 2001 hadi`2005, Nas aliusishwa katika ugomvi mkubwa na rapa mwenziwe Jay-Z. Marapa wote walikuwa wakishambuliana kwa kutumia nyimbo zao.

Wawili hao ugomvi wao ukaja kwisha baada ya kualikwa katika tamasha la muziki la New York City-area hip-hop za vituo vya redio. Nas akasaini mkataba na studio ya Jay-Z maarufu kama Def Jam mnamo mwaka 2006.

Albamu yake ya kwanza akiwa kama mmoja wa Def Jam, ilitoka mwaka wa 2006, ikiwa na jina la Hip Hop is Dead, ikiwa imeambatana na albamu nyingine ya mwaka wa 2008, iliyokwenda kwa jina la Untitled.[1]

Muziki

hariri

Albamu za muziki

hariri
Makala kuu ya: Albamu za Nas

Filamu

hariri
Mwaka Jina la filamu Jina alilotumia
2001 Sacred Is The Flesh kacheza kama "Isa Paige"
Ticker kacheza kama "Det. Art "Fuzzy" Rice"
1999 In Too Deep Alicheza kama Mwuza Madawa Kulevya katika Kona za Mtaa
1998 Belly kacheza kama "Sincere"

Marejeo

hariri
  1. "SoundCircuit.com: Artists: Tributes: Nas". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-03. Iliwekwa mnamo 2006-09-06.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: