Kleopatra

Kleopatra (* 69 KK; † 30 KK) alikuwa malkia wa mwisho wa Misri. Alipata elimu nzuri hadi kusema lugha nyingi kama vile Kikopti, Kiarabu, Kiaramo, Kihabeshi, Kifarsi na Kigiriki kama lugha ya mama.

Sarafu ya Kimisri yenye picha ya Kleopatra
Taswira ya 1660: Kifo cha Kleopatra

Malkia na fitinaEdit

Alipokuwa na miaka 18 babake Ptolemaio XII aliaga dunia akarithi ufalme pamoja na kakaye aliyekuwa mdogo wa miaka 12. Mwaka 49 KK washauri wa kaka walimfukuza Kleopatra katika ufalme. Alikaa jangwani kati ya makabila yaliyokuwa waaminifu naye hadi kuingia kwa Waroma nchini.

Kleopatra na CaesarEdit

Mwaka 48 vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Kiroma ilifika Misri. Pompeius adui wa Caesar alikimbilia Misri alipokamatwa na kuuawa na washauri wa mfalme. Julius Caesar mwenyewe alimfuata akajaribu kumaliza fitina ndani ya familia ya Kimisri. Alimpenda Kleopatra akamsaidia kushika ufalme tena. Akazaa mtoto naye aliyeitwa Caesarion (47 KK - 30 KK).

Caesar alirudi Roma na Kleopatra pamoja na mtoto alimfuata mwaka 44 alikuwako Roma wakati wa uuaji wa Caesar akarudi tena Misri.

Mke wa Marcus AntoniusEdit

Katika vita kati ya Marcus Antonius na Octavianus (Agusto wa baadaye) hakushikamana na pande lolote hadi kukutana na Marcus Antonius. Akawa mpenzi wake na Marcus alimfuata kuja Misri walipozaa watoto wawili. Marcus alimwacha nyuma alipoondoka Misri akarudi Roma mwaka 40 akapatana na Octavianus na kufunga ndoa na dada yake Octavia.

Mwaka 37 alipokuwa mtawala wa nusu ya mashariki ya dola la Roma alirudi kwa Kleopatra akamwoa mwaka 37 hata kama kisheria Mroma hakuruhusiwa kuwa na wake wengi. Katika agano lake Marcus aliwapa watoto wa Kleopatra majimbo katika mashariki.

33 BK Marcus Antonius alifarakana na Octavianus. Huyu alitumia nafasi ya kushawishi senati ya Roma kutangaza vita dhidi ya Misri kwa sababu ya majimbo yaliyokabidhiwa mkononi wa watoto wa Kleopatra.

Mwisho na kifoEdit

Katika mapigano ya Aktium meli za Octavianus zilishinda; Marcus Antonius alijiua. Baada ya kufika kwa Octavianus Misri malkia alijaribu kupatana naye ilyioshindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuonyeshwa kama mfungwa mbele ya watu wa mji. Hapa aliamua kuaga dunia tar. 12 Agosti 30 KK. Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake akamwua.