Nassoro Mohammed
Mwandishi wa Mashairi ya Kiswhaili
Nassoro Mohammed (anajulikana zaidi kama Mzee wa Khairati; alizaliwa Kilwa, 1946) ni mtunzi wa mashairi nchini Tanzania, akitunga mashairi katika lugha ya Kiswahili.
Ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mohamed Nassoro Mkutuka. Alizaliwa Kilwa na baadaye kuhamia katika mkoa wa Dar es Salaam. Baada ya baba yake kufariki dunia, mwaka 1960 alichukuliwa na kwenda kulelewa na shangazi yake akiwa na umri wa miaka 18.
Alianza kujifunza kazi mbalimbali kama upakaji rangi, lakini alipenda ushairi tangu akiwa bado mtoto mdogo.
Vitabu
haririMzee wa Khairati amechapisha diwani moja ya mashairi ya Kiswahili inayojulikana kama Diwani ya Khairati; diwani hiyo ilichapishwa mwaka 2019[1].
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nassoro Mohammed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |