Nice Mohamed
Nice Mohamed (amezaliwa 17 Aprili, 1973) ni mwigizaji, mwongozaji na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anafahamika sana kwa ushiriki wake katika mifululizo ya TV iliyokuwa inarushwa hewani na ITV chini ya Kaole Sanaa Group na jina maarufu la Mtunisi. Filamu alizocheza ni pamoja na: Tom Boy – Jike Dume, The Dream Ndoto, Kisasi cha Utata, Yellow Banana na Chanzo Kisu.[1]
Nice Mohamed | |
---|---|
Amezaliwa | Nice Mohamed 17 Aprili 1973 Tanzania |
Kazi yake | Mwigizaji Mwongozaji Mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 2001-hadi sasa |
Baadhi ya filamu zake
haririTazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Nice Mohamed Ilihifadhiwa 29 Mei 2017 kwenye Wayback Machine. katika Bongo Cinema
Viungo vya Nje
hariri- Nice Mohamed mahojiano katika Global TV - Youtube