Open main menu

Steven Charles Kanumba (alizaliwa tarehe 8 Januari 1984, Shinyanga - alikufa tarehe 7 Aprili 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.

Steven Kanumba
Steven-Kanumba.jpg
Hayati Steven Kanumba.
Amezaliwa Steven Charles Kanumba
Januari 8 1984 (1984-01-08) (umri 35) Shinyanga, Tanzania
Amekufa Aprili 7, 2012 (umri 28) Dar es Salaam, Tanzania
Kazi yake Muigizaji, Mtunzi, Mtayarishaji, Muongozaji

Maisha

Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.


Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.

Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.

Filmografia

Televisheni

  • Jahazi
  • Dira
  • Zizimo
  • Tufani
  • Sayari
  • Taswira
  • Gharika
  • Baragumu

Filamu

Mwaka Jina Maelezo
Haviliki
Neno
Ulingo
Riziki akiwa na Blandina Chagula
Sikitiko Langu akiwa na Nuru Nassoro, Vincent Kigosi, Ally Chaowa na Mahsein Awadh
Dangerous Desire akiwa na Vincent Kigosi, Nuru Nasoro and Blandina Chagula
She is My Sister akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus na Yvonne Cherryl
Penina akiwa na Mahsein Awadh, Emmanuel Myamba
Cross My Sin akiwa na Mercy Johnson, Suzan Lewis
2007 A Point Of No Return akiwa na Wema Sepetu, Mahsein Awadh
2008 The Lost Twins akiwa na Lucky Peter, Elizabeth Michael, Suzan Lewis
The Stolen Will akiwa na Eizabeth Chijumba, Immaculate Aloyce
Village Pastor akiwa na Aunt Ezekiel
Magic House akiwa na Nargis Mohamed, Issa Mussa
Oprah akiwa na Irene Uwoya na Vincent Kigosi
Red Valentine akiwa na Wema Sepetu, Jacquline Wolper
*Family Tears akiwa na Elizabeth Michael, Wema Sepetu na Richard Bezednhout
The Movie's Director akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus, Elizabeth Chijumba, Olufemi Ogdegbe
Fake Smile akiwa na Aunt Ezekiel, Yobnesh Yusuph
Unfortunate Love akiwa na Lisa Jensen, Aunt Ezekiel, Elizabeth Michael
Hero Of The Church akiwa na Princess Sheila, Issa Musa, Juma Kilowoko
Saturday Morning akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa
Shauku
Crazy Love akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa, Elizabeth Michael
2006 Johari[1] akiwa na Blandina Chagula na Vincent Kigosi)
2006 Dar 2 Lagos[1] akiwa na Mercy Johnson, Nancy Okeke, Bimbo Akintola
2010 More Than Pain akiwa na Lisa Jensen na Rose Ndauka
2010 Young Billionare akiwa na Aunty Ezekiel na Patcho Mwamba
2010 "Ripple of Tears" akiwa na Elizabeth Michael
2010 Uncle JJ
2010 This Is It
2010 Off Side akiwa na Irene Uwoya, Vincent Kigosi NA Jacob Steven
2010 Payback akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela
2010 Black Sunday akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela, Hemed Suleiman)
2010 Young Billionare akiwa na Aunty Ezekiel and Patcho Mwamba
2011 Saturday Morning akiwa na Irene Paul na Ben Franko
2011 Deception akiwa na Rose Ndauka, Patcho Mwamba, Bakari Makuka
2011 Devil Kingdom akiwa na Ramsey Noah, Kajala Masanja
2011 The Shock akiwa na Shazy Sadry
2011 Moses (filamu)Moses akiwa na Suzan Lewis, Shazy Sadri, Ndumbangwe Misayo
2012 Big Daddy
2012 Because of You akiwa na Rose Ndauka na Grace Mapunda
2012 Ndoa Yangu akiwa na Jacquline Wolper na Patcho Mwamba
2013 Love & Power akiwa na Irene Paul na Patcho Mwamba; filamu ya mwisho ya Kanumba

Marejeo

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steven Kanumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.