Nicole Scherzinger
Nicole Prescovia Elikolani Valiente Scherzinger[1] (pia anajulikana kama Nicole Kea) (amezaliwa tar. 29 Juni 1978) ni mwimbaji wa R&B, mtunzi wa nyimbo, mnenguaji, mwanamitindo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kuwa kama mwimbaji kiongozi wa kundi la muziki la The Pussycat Dolls. Amechekua jina la Scherzinger kwa sababu alilielewa na baba wa kufikia aliyekuwa Mjerumani.
Nicole Scherzinger | |
---|---|
Nicole mnamo Agosti 2012
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nicole Elikolani Prescovia Valiente |
Pia anajulikana kama | Nicole Kea |
Amezaliwa | 29 Juni 1978 Honolulu, Hawaii, Marekani |
Asili yake | R&B, hip hop, pop |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mnenguaji, mwigizaji, mwanamitindo |
Miaka ya kazi | 2001–hadi leo |
Studio | Polydor, A&M, Interscope |
Ame/Wameshirikiana na | Pussycat Dolls, Days of the New, Timbaland, Sean Combs, Keri Hilson, T.I., Will.I.Am, Sean Garrett, Will Smith, Nelly, Rihanna |
Tovuti | www.hernameisnicole.com |
Wasifu
haririMaisha ya awali
haririScherzinger alizaliwa mjini Honolulu, Hawaii na baba Mfilipino na mama Mhawaii/Mrusi.[2] Mama yake aliitwa Rosemary, na wakati ana mzaa Scherzinger alikuwa na umri wa miaka kumi na minane na wakawa wanaishi mjini inner city, lakini baadaye familia ikatengana wakati Scherzinger bado mdogo.
Baadaye familia ikaamia rasmi mjini Louisville, Kentucky wakati huo alikuwa na umri wa miaka sita, akiwa pamoja na ndugu yake wa kike aitwaye Ke'ala aliyezaliwa na baba Mjerumani Mwamerika Bw. Gary Scherzinger.[3][4]
Maisha binafsi
haririKwa sasa Scherzinger anatembea na Lewis Hamilton, kukiwa na fununu za kusema kuwa wawili hao wataoana punde.
Muziki
hariri- Tazama pia Eden's Crush na Albamu na Nyimbo za Pussycat Dolls kwa taarifa ya albamu na kazi alizofanya akiwa pamoja na hilo kundi.
Albamu
hariri- 2009: Her Name Is Nicole
Single
hariri- 2007: "Whatever U Like" akimshirikisha T.I.
- 2007: "Baby Love" akimshirikisha will.i.am
- 2007: "Supervillain" akimshirikisha Mad Scientist (Digital Release Only)
- 2007: "Puakenikeni" akishirikiana na Brick na Lace (Toleo la Mtandaoni Tu)
- 2008: "Rio" (Caress Brazilian Mix) (Toleo la Mtandaoni Tu)
Single alizoshirikishwa
hariri- 2006: "Lie About Us" (Avant akimshirikisha Nicole Scherzinger)
- 2006: "Come to Me" (Diddy akimshirikisha Nicole Scherzinger)
- 2007: "You Are My Miracle" (Vittorio akimshirikisha Nicole Scherzinger)
- 2008: "Scream" (Timbaland akimshirikisha Keri Hilson na Nicole Scherzinger)
Marejeo
hariri- ↑ Nicole Scherzinger.
- ↑ Nicole Scherzinger - Askmen.com.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-04. Iliwekwa mnamo 2008-11-10.
- ↑ "Pussycat Dolls Nicole She says she's 'only a 5 out of 10 for looks'". The Sun. Iliwekwa mnamo 2008-08-30.
Viungo vya nje
hariri- Official websiteArchived 3 Mei 2012 at the Wayback Machine.
- Kigezo:IMDb
- BMI.com repertoire search
- Errico, Mike. "25 Reasons to Love '07", Blender Magazine Online, Januari/Februari 2007. Retrieved on 2006-02-09. Archived from the original on 2007-09-30.
- nicole-scherzinger-2007-mtv-video-music-awards Archived 11 Januari 2009 at the Wayback Machine.