Nihoni
Nihoni (Nihonium) ni elementi ya kikemia yenye alama Nh na namba atomia 113. Iliitwa pia eka-thallium. Haitokei kiasili maana ni elementi sintetiki inayoweza kutengenezwa katika maabara kutokana na mbunguo wa Moskovi.
Elementi hii ilitambuliwa mwaka 2004. Vikundi vya wanasayansi waliitafuta wakati uleule pale Dubna (Urusi) na Wako (Japani). Hatimaye Wajapani walikubaliwa kuwahi kutambua tabia zake nyingi wakachagua jina kufuatana na jina la kienyeji cha Japani, "Nihon". [1] , [2] , [3]
Nusumaisha ya Nihoni ni sekunde chache, kwa hiyo haikudumu muda wa kutosha kuangalia tabia zake; kila kiasi kinachotengenezwa kinapotea baada ya sekunde kadhaa. Hivyo hakuna matumizi kwa elementi hiyo yanayojulikana.
Kulingana na nafasi yake katika jedwali la elementi inawezekana ni metali laini yenye rangi ya fedha ikiwa na utendanaji mkali wa kikemia.
Marejeo
hariri- ↑ Morita et al., Experiment on the Synthesis of Element 113 in the Reaction 209Bi(70Zn, n)278113 Ilihifadhiwa 5 Julai 2007 kwenye Wayback Machine., J. Phys. Ilihifadhiwa 1 Julai 2007 kwenye Wayback Machine.
- ↑ "press release in Japanese". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-01. Iliwekwa mnamo 2020-03-29.
- ↑ Japanese scientists create heaviest ever element
Tovuti za Nje
hariri- WebElements.com - Nihonium
- Uut na Uup Ongeza Misa yao ya Atomiki kwa Jedwali La Purela Ilihifadhiwa 7 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- Apsidium - Nihonium Ilihifadhiwa 15 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- Ugunduzi wa Vipengee 113 na 115 Ilihifadhiwa 23 Juni 2005 kwenye Wayback Machine.
- Ugunduzi wa Vipengele Vya Superheavy 113 na 115 Ilihifadhiwa 30 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- Vitu vya superheavy
- Nihonium kwenye Jedwali La Purela la Video (Chuo Kikuu cha Nottingham)
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nihoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |