Nilgai
Nilgai wanaocheza Uhindi (Boselaphus tragocamelus)
Nilgai wanaocheza Uhindi
(Boselaphus tragocamelus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Bovinae (Wanyama wanaofanana na ng'ombe)
Jenasi: Boselaphus (Nilgai)
de Blainville, 1816
Spishi: B. tragocamelus
(Pallas, 1766)
Msambao wa nilgai porini
Msambao wa nilgai porini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nilgai ni mnyama mkubwa wa pori wa spishi Boselaphus tragocamelus katika familia Bovidae. Huyo ndiye mnyama pekee katika jenasi Boselaphus.[1] Nilgai, anayeitwa nilgau pia, ndiye palahala mkubwa kabisa wa Asia. Ni mmoja wa wanyama pori wa kawaida kuonekana Uhindi ya kati na kaskazini, na huona mara nyingi katika ardhi ya shamba au pori. Madume wazima hufanana kidogo na ng'ombe, na hujulikana pia kama "fahali wa buluu". Nilgai wanaishi Uhindi na sehemu za Nepali ya kusini na Pakistani ya mashariki. Spishi hiyo imetoweka Bangladesh.

Maelezo

hariri
 
Nilgai wa kiume akipumzika katika nyasi.

Nilgai wana kimo cha mita 1.1–1.5 mabegani, urefu wa kichwa-mwili wa mita 1.7–2.1, na urefu wa mkia wa sm 45–50. Madume ni wakubwa kuliko majike, wakiwa na uzito wa kilo 109–288, hata hadi kilo 308, kulinganishwa na uzito wa majike wazima wa kilo 100–213.[1]

Nilgai ana miguu myembamba na mwili imara mwenye mgongo ambao wateremka chini kutoka mabegani. Muonekano wa madume na majike hutofautiana kiasi, lakini madume tu wana pembe. Madume wazima wana manyoya ya kijivu hadi kijivu-buluu, yenye madoadoa meupe kwenye mashavu na rangi ya nyeupe pia kando ya midomo. Pia wana mchirizi mwembamba mweupe toka koo kupita chini ya mwili, ulio mpana zaidi karibu na nyuma. Ncha za mkia mrefu na masikio ni nyeusi, na pia wana fungu la nywele ndefu za kukwaruza katika eneo la kati ya koo.[1]

Madume wana pembe nyeusi mbili zenye umbo la pia zitokazo kichwa kwa kukaribiana tu nyuma ya macho. Pembe hizo huendelea juu, lakini hupinda mbele kidogo; zina urefu wa sm 15–24 kwa nilgai mzima. Ingawa kwa kawaida pembe hizo ni laini, pembe za madume wazee zaidi zinaweza kuwa na migongo ya duara karibu na tako lao.[1]

Kwa upande mwingine, majike na watoto wana manyoya kahawia, ingawa vinginevyo wana alama zilinganazo na madume. Majike hawana pembe. Madume na majike wana manyoya ya wima nyuma ya shingoni yakimalizwa na vishungi juu ya mabegani.[1]

Hali ya sasa

hariri

Idadi ya nilgai Uhindi inakadiriwa kuwa takribani 100,000. Nilgai wa pori wanakuwepo pia katika majimbo ya Marekani ya Alabama, Florida, Mississipi na Texas, na jimbo la Meksiko la Tamaulipas, ambapo wametoroka mashamba binafsi ya mifugo.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Leslie, D.M. (2008). "Boselaphus tragocamelus (Artiodactyla: Bovidae)". Mammalian Species: Number 813: pp. 1–16.
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.