Pakistan
Pakistani ni nchi ya Asia ya Kusini. Imepakana na Ghuba ya Uarabuni upande wa kusini, Afuganistani na Uajemi upande wa magharibi, Uhindi upande wa mashariki na Uchina kaskazini-mashariki.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Iman, Ittehad, Tanzim (Kiurdu: "Imani, Umoja, Nidhamu") | |||||
Wimbo wa taifa: Pak sarzamin shad bad | |||||
Mji mkuu | Islamabad | ||||
Mji mkubwa nchini | Karachi | ||||
Lugha rasmi | Kiurdu, Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri ya Kiislamu Shirikisho la Jamhuri Arif Alvi Shehbaz Sharif | ||||
Uhuru Abbasiya Dola la Ghazni Ufalme wa Ghor Usultani wa Delhi Dola la Moghul imetangazwa Jamhuri |
kutoka Uingereza 711-962 962–1187 1187-1206 1210-1526 1526-1707 14 Agosti 1947 23 Machi 1956 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
881,912 km² (ya 36) 3.1 | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - Msongamano wa watu |
199,085,847 (ya 6) 260.08/km² (ya 55) | ||||
Fedha | Rupia (Rs.) (PKR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
PST (UTC+5:00) haipo (UTC+6:00) | ||||
Intaneti TLD | .pk | ||||
Kodi ya simu | +92
- |
Mipaka yake na Uhindi na Uchina haitambuliki kimataifa. Pakistan na Uhindi zote mbili zinadai eneo la Kashmir zikitawala kila moja sehemu za eneo hili.
Jina la Pākistān lina maana ya "nchi ya watu safi" kwa Kiurdu.
Pakistani ina nafasi ya sita kati ya nchi duniani zenye watu wengi.
Historia
haririWakati wa ukoloni
haririPakistani ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947.
Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858).
Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru.
Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".
Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Baada ya uhuru
haririTarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi.
Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.
Wakati ule ilikuwa nchi moja pamoja na Bangla Desh ya leo, lakini mwaka 1971 hizo pande mbili zilitengana baada ya vita kati yao.
Utawala
haririNchi ni shirikisho la majimbo manne ya Punjab, Sindh, Jimbo la mpaka wa kaskazini-magharibi na Baluchistan, mbali ya maeneo matatu.
Watu
haririLugha rasmi nchini Pakistan ni Kiurdu na Kiingereza. Lugha nyingine ni zaidi ya 60, lakini ni ndogo, zenye wasemaji wachache; karibu zote ni lugha za Kihindi-Kiulaya (angalia orodha ya lugha za Pakistan). Robo tatu za wakazi wanaelewa Kiurdu.
Asilimia 96.4 za wakazi ni Waislamu, hasa Wasuni. Ndiyo dini rasmi. Wahindu ni 2.14% na Wakristo 1.27%.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti rasmi
- Pakistan entry at The World Factbook
- Pakistan Archived 29 Agosti 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Pakistan katika Open Directory Project
- Pakistan from the BBC News
- Pakistan at Encyclopædia Britannica
- Wikimedia Atlas of Pakistan
- Key Development Forecasts for Pakistan from International Futures
- Population Of Pakistan Archived 2 Julai 2014 at the Wayback Machine.
- World Bank Pakistan Summary Trade Statistics
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Pakistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |