Senene
Senene | ||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Jika la Ruspolia nitidula anayefanana na senene
| ||||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||||
|
Senene (jina la kisayansi: Ruspolia differens[1] [2]; jina la Kiganda: Nsenene; jina lililokosewa: "panzi wenye pembe ndefu") ni mdudu wa familia Tettigoniidae katika oda Orthoptera. Wapo tele magharibi mwa Kenya na Tanzania, kusini mwa Uganda na kaskazini mwa Rwanda lakini anapatikana pia Afrika Kusini, Malawi, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Burundi, Kamerun, Zimbabwe, Zambia, Madagaska pamoja na Mauritius.[3]
Baada ya majira ya mvua wapevu hukongomana katika makundi ya maelfu ya wadudu.
Spishi aina hii kwa muda mrefu imekuwa ikijulikana kama moja ya totems nyingi za Ufalme wa Buganda wa Uganda. Zilipatikana na Seruwu Douglass kutoka Visiwa vya Ssese huko Masaka.
Mara nyingi wadudu kama senene huitwa panzi, lakini senene wana vipapasio virefu sana kuliko pronoto na jike ana kiungo kama mfuo kinachofanana na kitara kinachotumika kwa kutaga mayai. Kinyume na hivyo panzi wana vipapasio vifupi na majike hawana kiungo kwa umbo la kitara.
Mara nyingi huchanganyikiwa na Ruspolia nitidula inayohusiana kwa karibu.[4][5]
Kama chakula
haririWakati wapevu wa senene wakionekana watu huajili kuwakusanya ili kuwakaanga kama chakula. Nchini Uganda senene walikamatwa kwa desturi na wanawake na watoto. Baada ya kukaangwa chakula hiki kilitolewa kwa waume wa wanawake wale kwa malipo ya gomasi mpya (Kiganda: gauni ya kitamaduni). Ingawa wanawake walilazimishwa kufanya kazi hiyo ya kuchosha hawakuruhusiwa kula chakula hiki. Iliaminika kwamba wanawake wanaokula senene wangezaa watoto wenye kichwa cha umbo la kichwa cha senene. Siku hizi wanawake hula senene bila shida.
Nchini Tanzania chakula cha senene hupendwa sana na watu wa Bukoba, hasa kabila la Wahaya, na katikati na kusini-magharibi mwa Uganda, kikiwa pia chanzo muhimu cha mapato.
Marejeo
hariri- ↑ "species Ruspolia differens (Serville, 1838): Orthoptera Species File". orthoptera.speciesfile.org. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
- ↑ Ssepuuya, Geoffrey; Wynants, Enya; Verreth, Christel; Crauwels, Sam; Lievens, Bart; Claes, Johan; Nakimbugwe, Dorothy; Van Campenhout, Leen (2019-02-01). "Microbial characterisation of the edible grasshopper Ruspolia differens in raw condition after wild-harvesting in Uganda". Food Microbiology (kwa Kiingereza). 77: 106–117. doi:10.1016/j.fm.2018.09.005. ISSN 0740-0020.
- ↑ academic.oup.com https://academic.oup.com/jee/article-abstract/115/3/724/6582281?redirectedFrom=fulltext&login=false. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
{{cite web}}
: Missing or empty|title=
(help) - ↑ Matojo, Nicodemus D.; Hosea, Keneth M. (2013-05-21). "Phylogenetic Relationship of the Longhorn Grasshopper Ruspolia differens Serville (Orthoptera: Tettigoniidae) from Northwest Tanzania Based on 18S Ribosomal Nuclear Sequences". Journal of Insects (kwa Kiingereza). 2013: e504285. doi:10.1155/2013/504285. ISSN 2356-7465.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ academic.oup.com https://academic.oup.com/jee/article-abstract/113/5/2150/5892968?redirectedFrom=fulltext&login=false. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
{{cite web}}
: Missing or empty|title=
(help)