Ntobeye ni miongoni mwa kata za Wilaya ya Ngara katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35704 [1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 17,003 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,758 waishio humo.[3]

Ntobeye ina maeneo pendwa kwa wakazi wa kata hiyo. Maeneo hayo ni kama vile: Nyakariba, Mutukura, Nyamisagara, Mukinengo, Burambira, Runzenze, Chivu, Mukatoketoke na maeneo mengine zaidi.

Nyakariba ni sehemu maarufu kwa wakazi wa Ntobeye. Jina hili linaenziwa kwa kuwa na shule inayoitwa Nyakariba Primary School. Jina la eneo hili lilitokana na kisima kidogo cha asili kilichokuwa kinaitwa Iriba kilichotegemewa sana na wakazi wa eneo hilo enzi za wahenga. Mpaka sasa Nyakariba ina wakazi wanaojihusisha na kilimo, ufugaji na uwindaji. Nyakariba si kijiji, lakini inafahamika kwa kuwa na vitongoji viwili maarufu: Kumulenge na Gwintuku.

Wenyeji wa eneo hili wanapenda wageni na ni wakarimu kwa asili.

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 175
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Ngara-District-Council
  Kata za Wilaya ya Ngara - Mkoa wa Kagera - Tanzania  

Bugarama | Bukiriro | Kabanga | Kanazi | Kasulo | Keza | Kibimba | Kibogora | Kirushya | Mabawe | Mbuba | Muganza | Mugoma | Murukurazo | Murusagamba | Ngara Mjini | Ntobeye | Nyakisasa | Nyamagoma | Nyamiaga | Rulenge | Rusumo


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ntobeye kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.