Nungwi
Nungwi ilikuwa kata ya Wilaya ya Unguja Kaskazini 'A' katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Tanzania inakadiriwa kupatikana maili 36 (kilomita 56) kaskazini mwa mji wa Zanzibari, katika rasi ya Nungwi, kama mwendo wa saa moja kwa gari kutoka Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,916 waishio humo. [1]
Nungwi inajulikana pia kama "Ras Nungwi"[2] maana inapatikana kwenye rasi iliyo ncha ya kaskazini ya kisiwa cha Unguja. Katika miaka tangu mnamo mwaka 2000 Nungwi imekuwa moja kati ya vitovu vya utalii vya Unguja.
Ni kijiji kikubwa kinachopatikana kaskazini ya mbali ya visiwa vya Zanzibar ambacho kinaweza kuwa kidogo kuliko eneo la Makunduchi.[3]
Historia
haririKulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale katika pwani ya Bahari ya Hindi.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Ripoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-12-28.
- ↑ http://gobackpacking.com/nungwi-village-zanzibar/
- ↑ http://gobackpacking.com/nungwi-village-zanzibar/
Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nungwi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |