Zanzibar (maana)
ukarasa wa maana wa Wikimedia
(Elekezwa kutoka Zanzibari)
Zanzibar ni neno linalotaja
- Kijiografia Funguvisiwa la Zanzibar kwenye mwambao wa Afrika ya Mashariki hasa visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo
- Nje ya Tanzania kisiwa cha Unguja mara nyingi huitwa "Zanzibar"
- Kihistoria Usultani wa Zanzibar iliyoanzishwa baada ya kifo cha Sultani Sayyid Said na kugawiwa kwa Usultani wa Omani mwaka 1856 wakati mwanaye Sayyid Majid alipokuwa sultani wa kwanza wa Zanzibar akitawala funguvisiwa la Zanzibar pamoja na pwani ya Afrika ya Mashariki kati ya Mogadishu (leo mji mkuu wa Somalia) na Rasi Delgado (leo Msumbiji ya Kaskazini karibu na mto wa Ruvuma).
- Kisiasa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Zanzibar ilipata uhuru kwa njia ya mapinduzi mwaka 1963 na iliungana na Tanganyika mwaka 1964 hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na waasisi walikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Zanzibar ina jumla ya mikoa mitano ambayo ni: Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba
- Jiji la Zanzibar ambalo ni mji mkubwa wa Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
- Jina la filamu, vitabu, hoteli n.k. zilizotajwa kufuatana na neno lenyewe kama vile Jamhuri ya Zanzibar, funguvisiwa la Zanzibar, jiji la Zanzibar n.k.
- Kuhusu maana ya neno lenyewe taz. "Etimolojia ya Neno Zanzibar" .