Hamidu Salim Chambuso (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dogo Hamidu na baadaye Nyandu Tozzy; amezaliwa 2 Julai 1987) ni msanii wa muziki wa rap kutoka nchini Tanzania,

Nyandu alianza muziki mwishoni mwa miaka ya 2000 na amewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Tanzania akiwa ni pamoja na Profesa Jay, Soggy Doggy Hunter, Unique Sisters, Taff B., Young Dee mara mbili katika "Nimekasirika (2012) na "Double Double[1]" (2017), Fid Q[2], Dudu Baya, Chin Bees, Mr. Blue akiwa kama mwanachama mwenza katika kundi la B.O.B Click.

Katika kazi yake ya muziki, amewahi kuwa sehemu ya kundi la muziki la "New Jack Family" kabla ya hapo alikuwa na akina Slim ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la CBM Crew. Baadaye alisimama muziki lakini alivyorudi tena, wakaanzisha B.O.B Micharazo akiwa na Mr. Blue, Becka Title, Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege, na wasanii wengine.

Marejeo hariri

  1. "Pin on Audio | Nyandu Tozzy ft. Young Dee , Chin Bees – Double Double | Mp3 Download". Pinterest (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-27. 
  2. djmwanga (2021-04-08). "AUDIO | Nyandu Tozzy Ft. Fid Q & Mbosso – 26 Life | Download". DJ Mwanga (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-04-27. 

Viungo vya nje hariri