Nyokachungwa
Kimanjano (Telescopus semiannulatus)
Kimanjano (Telescopus semiannulatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Jenasi: Telescopus
Wagler, 1830
Ngazi za chini

Spishi 14:

Nyokachungwa ni spishi za nyoka wenye sumu wa jenasi Telescopus katika familia Colubridae. Spishi 9 zinapatikana katika Afrika na spishi 5 katika Eurasia tu.

Nyoka hawa ni warefu kiasi, kwa wastani sm 80-180 lakini. Rangi ya spishi kadhaa za Afrika ni machungwa na zote zina mabaka meusi. Spishi nyingine ni kijivu au kahawia pamoja na mabaka.

Nyokachungwa huwinda usiku na kwa hivyo macho ni makubwa kiasi. Nyinging huishi mitini, nyingine ardhini. Hula mijusi hasa lakini spishi nyingine hukamata ndege wadogo, panya na amfibia pia.

Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa. Kwa kawaida hawaingizi sumu waking'ata mtu lakini kwa nadharia wanaweza kuifanya na hung'ata mara nyingi wakishikwa. Kwa hivyo inashauriwa kushughulikia nyoka hawa kwa makini

Spishi za Afrika hariri

Spishi za mabara mengine hariri

Picha hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyokachungwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.