Wakartusi
Shirika la Wakartusi, au Shirika la Mt. Bruno, ni utawa mmojawapo wa Kanisa Katoliki. Wamonaki wake wote, wanaume kwa wanawake wanaishi ndani kwa ndani: wengine katika nyumba za binafsi, wengine katika makao ya pamoja.
Shirika lilianzishwa na Bruno Mkartusi mwaka 1084.
Linafuata sheria zake, badala ya kanuni ya Benedikto wa Nursia inayoongoza wamonaki karibu wote wa Kanisa la Kilatini.
Jina linatokana na milima ya Chartreuse (nchini Ufaransa), ambapo Bruno na wakaapweke wenzake 6 walijenga makao ya kwanza.
Kaulimbiu ya shirika ni: Stat crux dum volvitur orbis (kwa Kilatini "Msalaba unadumu wakati ulimwengu unabadilikabadilika."
Hatua upwekeni
hariri- Utakaji (miezi 3 hadi 12).
- Unovisi (miaka 2).
- Nadhiri za muda (miaka 3).
- Nadhiri za daima.
Nyumba za Wakartusi leo
haririLeo duniani ziko nyumba 25 za Wakartusi; kati yake 5 ni za masista. Kwa jumla wako wamonaki 370 wanaume na 75 wanawake. Monasteri hizo ziko Argentina (1), Brazil (1), France (6), Germany (1), Italy (4), Ureno (1), Slovenia (1), South Korea (2), Spain (5), Uswisi (1), Ufalme wa Muungano (1) na Marekani (1).[1]
Filamu
hariri- "Into Great Silence"—the award winning documentary on the hermit monks of the Roman Catholic Carthusian Order
Tanbihi
hariri- ↑ To view complete list and images of the Monasteries visit: "The charterhouses in the world". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-10-20. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2010.
Marejeo
hariri- Lockhart, Robin Bruce. Halfway to Heaven. London:Cistercian Publications, 1999 (Paperback,ISBN 0-87907-786-7)
- The Wound of Love, A Carthusian miscellany by priors and novice masters on various topics relating to the monastic ideal as lived in a charterhouse in our day. Gracewing Publishing, 2006, 256 p. (paperback, ISBN 0852446705)
- André Ravier, Saint Bruno the Carthusian. Online on the website of the Charterhouse of the Transfiguration Ilihifadhiwa 12 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- Klein Maguire, Nancy. An Infinity of Little Hours: Five Young Men and Their Trial of Faith in the Western World's Most Austere Monastic Order. PublicAffairs, 2006 (Hardcover,ISBN 1-58648-327-2)
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya shirika
- International Fellowship of St. Bruno
- Article from the Catholic Encyclopedia
- Cartusiana - Historia ya Wakartusi huko Uholanzi
- Tovuti rasmi ya Wakartusi wa Roermond, Uholanzi
- Tovuti rasmi ya filamu "Into Great Silence"
- Slant Magazine Film Review by Keith Uhlich
- U.S. distributor: Zeitgeist films - includes 12 page press kit, downloadable Ilihifadhiwa 16 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.
- Movie Review at the Vivificat! Blog