Paoneaanga
(Elekezwa kutoka Observatory)
Paoneaanga (pia: kituo cha nyota, kituo cha astronomia; kwa Kiingereza: astronomical observatory) ni taasisi ya kuangalilia anga na magimba yake kama vile jua, mwezi, nyota, sayari, kometi au galaksi.
Kwa kawaida ni jengo lenye darubini kubwa. Mara nyingi hujengwa juu ya mlima au mbali na miji kwa kusudi la kupunguza athari za machafuko wa hewa au wa nuru za makazi. Ni muhimu kupunguza athari zinazoleta ugumu wa kuona vema mwanga hafifu wa nyota.
Kabla ya kugunduliwa kwa darubini, kulikuwa na majengo maalumu ya kuangalia hasa mahali ambako Jua au nyota fulani iliweza kutazamiwa kuonekana siku maalumu na hii ilikuwa muhimu kwa kukadiria kalenda.
Siku hizi kazi ya paoneanga duniani inasaidiwa na kupanushwa na darubini kwenye anga-nje.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paoneaanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |