Kiolwa cha angani

(Elekezwa kutoka Gimba la angani)

Kiolwa cha angani (pia: gimba la angani, kwa Kiingereza: astronomical object au celestial body) ni jina la jumla kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu.

Asteroid Ida with its own moonMimas, a natural satellite of Saturn
Planet Jupiter, a gas giant
The Sun, a G-type starStar Sirius A with white dwarf companion Sirius B
Black hole (artist's animation)Vela pulsar, a rotating neutron star
Globular star clusterPleiades, an open star cluster
The Whirlpool galaxyAbel 2744, Galaxy cluster
The Hubble Ultra-Deep Field 2014 image with an estimated 10,000 galaxiesMap of galaxy superclusters and filaments
Mifano ya violwa vya angani

Kwa Kiingereza istilahi "object" (kiolwa) na "body" (gimba) mara nyingi hutumiwa kama visawe. Lakini ilhali kila gimba la anga-nje ni pia kiolwa cha anga-nje, kinyume chake si kweli. Gimba la anga-nje ni kitu kimoja cha pekee, kama vile sayari, mwezi, asteroidi. Kiolwa cha anga-nje ni wazo pana zaidi, likitaja pia mambo kama galaksi au nebula yenye sehemu nyingi ndani yake.

Kati ya violwa vya anga-nje huhesabiwa:

Hivyo vyote ni violwa asilia. Vitu vilivyoko kwenye anga-nje vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya anga-nje. Hapa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombo vya anga-nje vilivyovunjika au takataka ya angani yanayotokana na safari za anga-nje yanastahili kuitwa kwa neno hili.

Elimu ya violwa vya anga-nje ni astronomia.

Makala hii kuhusu "Kiolwa cha angani" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiolwa cha angani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.