Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo
Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo (kwa Kiingereza: obsessive-compulsive disorder, kifupi: OCD[1]) ni tatizo la akili ambapo mtu huhisi haja ya kuangalia vitu mara kwa mara, kufuata utaratibu fulani mara kwa mara, au kuwa na mawazo yaleyale mara kwa mara.[2] Watu hao hawana uwezo wa kudhibiti ama mawazo au shughuli kwa zaidi ya kipindi kifupi. [2] Shughuli za kawaida ni kama vile kuosha mikono, kuhesabu vitu, na kuangalia iwapo mlango umefungwa.[2] Wengine wanaweza kuwa na ugumu wa kutupa vitu nje.[2] Shughuli hizo hutokea kiasi kwamba maisha ya kila siku yanaathirika vibaya.[2] Hii mara nyingi hutokea zaidi ya saa moja kwa siku.[3]
Watu wazima wengi hugundua kwamba tabia hizo hazina maana.[2] Hali hiyo inahusiana na mitetemo ya neva usoni, tatizo la kuwa na wasiwasi kila mara, na kuongezeka kwa hatari ya kujiua.[3][4]
Chanzo
haririChanzo hakijulikani[2] ila kuna visababishi fulani vya jenetikia, hivyo pacha wanaofanana huathiriwa sana mara nyingi kuliko pacha wasiofanana.[3] Vipengele vya hatari ni kama vile historia ya unyanyasaji wa mtoto au tukio linalosababisha mawazo mazito.[3] Baadhi ya hali zimeshawekwa kwenye kumbukumbu kutokea kwa sababu ya maambukizi.[3] Utambuzi unategemea dalili na huhitaji kuondoa vyanzo vingine vinavyohusiana na dawa au tiba.[3]
Vipimo vya viwango kama vile Yale–Brown Obsessive Compulsive Scale (Y-BOCS) vinaweza kutumika ili kutathmini ukali wake.[5]
Matatizo mengine yaliyo na dalili sawa ni pamoja na tatizo la kuwa na wasiwasi kila mara, tatizo la kuwa na huzuni kali kwa muda mrefu, tatizo la kula isivyo kawaida, tatizo la kuwa na mtetemo wa neva usoni, na tatizo la akili linalomfanya mtu kurudiarudia tabia fulani ya kibinafsi.[3]
Tiba
haririMatibabu yanajumuisha ushauri, kama vile tiba ya tabia za utambuzi (CBT), na wakati mwingine dawa za kutibu huzuni kama vile kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs) au dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine).[6][7]
Tiba ya tabia za utambuzi (CBT) kwa tatizo hili (OCD) huhusisha kuongeza kuwekwa wazi kwa chanzo cha shida huku huruhusu tabia ya kujirudia kutotokea.[6] Huku dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine) huonekana kufanya kazi sawa na kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs), ina madhara mengi hivyo huachwa kwanza ili itumike kukihitajika tu.[6] Dawa za kutibu magonjwa ya kisaikolojia zisizo za kawaida zinaweza kuwa muhimu zikitumika pamoja na SSRI katika hali za kukataa matibabu lakini pia zinahusishwa na hatari ya ongezeko la madhara.[7][8] Bila matibabu, hali hiyo mara nyingi hudumu kwa miongo.[3]
Uenezi
haririTatizo hili huathiri karibu 2.3% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao.[9] Viwango katika mwaka fulani ni karibu 1.2%, na hutokea kote ulimwenguni.[3] Si kawaida kwa dalili kuanza baada ya umri wa miaka 35, na nusu ya watu huwa na matatizo kabla ya umri wa miaka 20.[2][3] huku wanaume na wanawake huathiriwa kwa viwango sawa.[2]
Tanbihi
hariri- ↑ Katika Kiingereza, kirai kuwa na hofu na kurudia kitu (obsessive-compulsive) mara nyingi hutumika kwa njia isiyo rasmi isiyohusika na Tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani (OCD) kuelezea mtu ambaye mwangalifu sana katika mambo madogo madogo, mkamilifu, ametekwa fikra, au vinginevyo kufungwa kwa kitu au mtu. Taz. Bynum, W.F.; Porter, Roy; Shepherd, Michael (1985). "Obsessional Disorders: A Conceptual History. Terminological and Classificatory Issues.". The anatomy of madness : essays in the history of psychiatry. London: Routledge. ku. 166–187. ISBN 978-0-415-32382-6.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 2.8 The National Institute of Mental Health (NIMH) (Januari 2016). "What is Obsessive-Compulsive Disorder (OCD)?". U.S. National Institutes of Health (NIH). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 24 Julai 2016.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (tol. la 5). Washington: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 237–242. ISBN 978-0-89042-555-8.
- ↑ Angelakis, I; Gooding, P; Tarrier, N; Panagioti, M (25 Machi 2015). "Suicidality in obsessive compulsive disorder (OCD): A systematic review and meta-analysis". Clinical Psychology Review. 39: 1–15. doi:10.1016/j.cpr.2015.03.002. PMID 25875222.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fenske JN, Schwenk TL (Agosti 2009). "Obsessive compulsive disorder: diagnosis and management". Am Fam Physician. 80 (3): 239–45. PMID 19621834. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Mei 2014.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ 6.0 6.1 6.2 Grant JE (14 Agosti 2014). "Clinical practice: Obsessive-compulsive disorder". The New England Journal of Medicine. 371 (7): 646–53. doi:10.1056/NEJMcp1402176. PMID 25119610.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 Veale, D; Miles, S; Smallcombe, N; Ghezai, H; Goldacre, B; Hodsoll, J (29 Novemba 2014). "Atypical antipsychotic augmentation in SSRI treatment refractory obsessive-compulsive disorder: a systematic review and meta-analysis". BMC Psychiatry. 14: 317. doi:10.1186/s12888-014-0317-5. PMC 4262998. PMID 25432131.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Decloedt EH, Stein DJ (2010). "Current trends in drug treatment of obsessive-compulsive disorder". Neuropsychiatr Dis Treat. 6: 233–42. doi:10.2147/NDT.S3149. PMC 2877605. PMID 20520787.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Goodman, WK; Grice, DE; Lapidus, KA; Coffey, BJ (Septemba 2014). "Obsessive-compulsive disorder". The Psychiatric clinics of North America. 37 (3): 257–67. doi:10.1016/j.psc.2014.06.004. PMID 25150561.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo katika Open Directory Project
- National Institute Of Mental Health
- American Psychiatric Association
- APA Division 12 treatment page for obsessive-compulsive disorder
- Davis, Lennard J. (2008). Obsession: A History. University of Chicago Press. ISBN 978-0-226-13782-7.