Ohio (mto)
Mto Ohio ni tawimto muhimu wa mto Mississippi katika mashariki ya Marekani.
Urefu wake ni kilomita 1,579 kuanzia chanzo chake kwenye maungano ya mto Allegheny na mto Monongahela karibu na mji wa Pittsburgh hadi mdomo kwenye mto Mississippi. Njia ya mto ni mpaka kati ya majimbo sita ya Marekani na beseni yake inajumlihsa eneo la majimbo 14. Tawimto kubwa ya kuingia ni mto Tenessee.
Katika historia ya Marekani ilikuwa njia muhimu ya mawasiliano kabla ya kujengwa kwa barabara na reli. Wakati wa karne ya 19 Ohio ilikuwa mpaka kati ya maeneo yaliyoruhusu utumwa na majimbo yaliyokataa utumwa.
Mto huu umepakana na majimbo ya Ohio, Kentucky, Illinois, Indiana, West Virginia na Pennsylvania. Miji muhimu kando la mto ni Louisville, Kentucky, Paducah, Kentucky, Cincinnati, Ohio na Pittsburgh, Pennsylvania.
Viungo vya Nje
hariri- Historic Ohio, the magazine Archived 15 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- Ohio Historical Preservation Group Archived 27 Machi 2009 at the Wayback Machine.
- Ohio River Valley Families Online Searchable Database, a genealogy resource
- Image at the confluence with the Mississippi River
- Watershed information Archived 26 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
- Ohio River Forecast Center, which issues official river forecasts for the Ohio River and its tributaries
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ohio (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |