OpenAI ni kampuni ya Marekani inayofanya tafiti na utoaji huduma wa akili bandia. Ilianzishwa na kundi la wajasiriamali, wawekezaji, na watafiti mashuhuri mnamo Desemba 2015. Lengo kuu la kampuni hii ni kuhakikisha akili bandia ya jumla (akili bandia yenye uwezo wa kiakili mkubwa kuliko binadamu) inawanufanisha binadamu wote kwa ujumla, kuzuia hatari zinazotishia uwepo wa binadamu pamoja na matumizi mengine mabaya.

OpenAI inc
Pahali pa makao makuuSan Francisco, California Marekani
Watu muhimuBret Taylor (Mwenyekiti), Sam Altman (Mkurugenzi). Greg Brockman (Rais), Ilya, Sutskever (Mkurugenzi mipango), Mira Murati (Mkurugenzi teknolojia)
Sekta ya viwandaTeknolojia ya habari
BidhaaGPT-1, GPT-2, GPT-3, GPT-4, ChatGPT, DALL·E, OpenAI Five, OpenAI Codex
MapatoDola za marekani bilioni 1.6 (2023) [1]
FaidaDola za marekani bilioni 86 (2023) [2]
MmilikiMicrosoft (49%)
Wafanyakazi201-500 (2023) [3]
Tovutihttps://openai.com/
Tarehe ya uzinduziDesemba 11, 2015; miaka 8 iliyopita (2015-12-11)

Kampuni inajiendesha kama "shirika la faida iliyopunguzwa" (kiingereza capped-profit entity), kwa kuzuia kiasi cha faida kinachopata kwenye bidhaa na huduma zake huku ikiongozwa na shirika baba lisilo la kifaida linalosimamia na kuongoza malengo na shughuli zake [4].[5][6]

OpenAI inasifika kwa tafiti zake zilizovunja rekodi kwenye akili bandia haswa kwenye tawi la usindikaji wa lugha ya asili, maono ya kompyuta (kiingereza: computer vision) na mafunzo ya kujiimarisha (kiingereza: reinforcement learning). Baadhi ya bidhaa zao zilizopata umaarufu zaidi ni roboti la mazungumzo la ChatGPT, mfumo wa akili bandia ya kuzalisha picha ya DALL·E, na OpenAI Codex, mfumo wa kuandika misimbo chanzo ya kompyuta ya kiwango cha juu kwa kutumia maelekezo ya lugha asilia.

Marejeo

hariri
  1. https://www.reuters.com/technology/openai-annualized-revenue-tops-16-billion-information-2023-12-30/
  2. https://www.bloomberg.com/opinion/articles/2023-11-27/openai-is-still-an-86-billion-nonprofit
  3. https://www.linkedin.com/company/openai
  4. "Understanding the Concept: OpenAI's Capped Profit Model". www.upstock.io (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-12. Iliwekwa mnamo 2024-01-12.
  5. "OpenAI LP". openai.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-12.
  6. "What is unusual about OpenAI's board structure and how does it differ from for-profit entities?". Quora (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-12.
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu OpenAI kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.