Osmani I
(Elekezwa kutoka Osman I)
Osmani I (1258–1326) alikuwa mwanzilishaji wa Waosmani aliyeweka msingi kwa Milki ya Osmani iliyoendelea kwa karne sita hadi 1922 katika eneo la Uturuki, Balkani, Shamu na Misri.
Chanzo chake ilikuwa kama chifu au mtemi wa kabila la Kiturki mpakani wa Ufalme wa Bizanti katika Anatolia. Awali utemi wake ilikuwa chini ya Waturki Waselchuki lakini baada ya uvamizi wa Wamongolia mnamo 1258 uwezo wa Waselchuki ulipungua na Osman alijitangaza kuwa Sultani wa dola huru mwaka 1299.
Aliendelea kuwashambulia hasa Wabizanti kwa msaada wa maghazi wengi waliojiunga naye kutoka nchi mbalimbali za Waislamu kwa kusudi la kuendesha vita ya jihadi.
Alipoaga dunia eneo lake lilikuwa limepanuka kutoka kilomita za mraba 4,800 kuwa 16,000.