Panagia (kutoka Kigiriki: Παναγία, Mtakatifu kabisa) ni jina la heshima kwa Bikira Maria, mama wa Yesu, linalotumika hasa katika Ukristo wa Mashariki. Linasisitiza utakatifu wake uliozidi ule wa binadamu wengine wote, isipokuwa Mwanae.

Panagia kutoka Yaroslavl, karne ya 13.

Jina hilo linatumika pia kwa aina maalumu ya picha takatifu za Mama wa Mungu zinazomuonyesha akisali huko akimuelekea mtazamaji kama uso kwa uso na kuwa na Mwanae amechorwa katika duara kifuani mwake[1].

Tanbihi hariri

  1. Great Panagia, History of Russian Painting, by Boguslawski

Marejeo hariri

  • The Blackwell Dictionary of Eastern Christianity, p. 368 (ISBN|0-631-23203-6)