Paoneaanga pa Mount Palomar

Paoneaanga pa Mount Palomar ni kituo cha kuangalilia nyota kinachopatikana kwenye kimo cha mita 1706 juu ya milima ya Palomar takriban kilomita 80 upande wa kaskazini wa San Diego kwenye jimbo la Kalifornia, Marekani.

Mnara wa darubini, paoneanga pa Mt Palomar
Kioo parabola cha Hale jinsi kilivyosagwa mwaka 1945

Paoneaanga hapo palikuwa maarufu kwa sababu kuna darubiniakisi yenye kioo parabola cha kipenyo cha mita 5 (inchi 200). Katika miaka ya 1948 hadi 1975 hiyo ilikuwa darubini kubwa kuliko zote duniani. Kioo parabola chake kina uzito wa tani 13, darubini yote ina tani 400[1].

Darubini hii inaitwa "Hale Telescope" kwa heshima ya George Hale aliyeunda kituo cha Munt Palomar. Iliwezesha wanaastronomia kugundua violwa vya mbali sana pamoja[2] na kuonyesha nyota ndani ya galaksi. Maelfu ya asteroidi zilitambuliwa ka kutumia darubini ya mt Palomar. Vilevile magimba katika Ukanda wa Kuiper yalitambuliwa pamoja na sayari kibete Makemake.

Marejeo

  1. The 200-inch (5.1-meter) Hale Telescope, tovuti ya taasisi ya Caltech
  2. How far can the Hale telescope see?, tovuti ya Caltech, FAQ