Wanaastronomia

Wanaastronomia ni wataalamu wa masuala ya astronomia (kwa Kiingereza: astronomy) au elimu ya nyota na anga-nje.

Mwanaastronomia wa kihistoria akipima pembe baina ya nyota kwa kutumia sudusi

Kihistoria watu hao walitumia muda mwingi kuangalia nyota za anga kwa msaada wa vyombo kama darubini. Leo hii wanaastronomia hutumia hasa kompyuta na data kutokana na vipimo vya paoneaanga, vyombo vya anga-nje na darubini za angani.

Wanaastronomia wamesoma astronomia ambayo ni tawi la pekee la sayansi, mara nyingi pamoja na kusoma matawi mengine ya sayansi kama fizikia, kemia, biolojia na kadhalika.

Wasichanganywe na majusi ambao husomea unajimu (kwa Kiingereza: astrology) na kutoa utabiri kuhusu maisha na tabia za watu kwa kuwa huo si tawi la sayansi yoyote, ingawa unadai kutegemea uchunguzi wa nyota n.k.

Atom editor logo black.svg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanaastronomia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano