Patrick Agyemang

Mwanasoka wa Ghana

Patrick Agyemang (alizaliwa Walthamstow, Uingereza, 29 Septemba, 1980, alikuwa mchezaji wa kandanda wa timu ya taifa ya Ghana.

Patrick Agyemang
Maelezo binafsi
Jina kamili Patrick Agyemang
Tarehe ya kuzaliwa 29 Septemba 1980
Mahala pa kuzaliwa    Walthamstow, Uingereza
Urefu 1.85m
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Queens Park Rangers F.C.
Namba 11
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1998–2004
1999–2000
2004
2004–2008
2008-
Wimbledon FC
Brentford FC
Gillingham FC
Preston North End FC
Queens Park Rangers
Timu ya taifa
2003–2006 Ghana

* Magoli alioshinda

Historia

hariri

Amechezea timu yake ya taifa mechi mbili. Yeye sasa anacheza katika klabu ya Queens Park Rangers katika michuano ya Ligi ya Soka ya daraja la tatu huko Uingereza.

Klabu za zamani za Agyemang ni Preston North End na Wimbledon.

Wasifu wa Klabu

hariri
 
Uwanja wa Deepdale,uwanja wa Preston North End,ambako Agyemang alicheza misimu minne na kufunga mabao

Wasifu wake akiwa Preston North End na klabu zingine za awali

hariri

Agyemang alijiunga na klabu ya Preston North End katika mkataba uliokuwa na gharama ya takriban £ 300,000 kutoka Gillingham baada ya kuwa Priestfield kwa muda usiofika mwaka mmoja.

Mshambulizi huyoa alipata umaarufu akiwa Wimbledon ambako alikua na akacheza mechi 116 na kufunga mabao 22.

Agyemang alicheza mechi31 katika msimu wake wa kwanza huku akifunga mabao manne lakini bado akaorodheshwa kama ako chini ya Nugent na Cresswell katika timu hiyo.

Msimu huu, mshambulizi huyu amecheza mechi 49 ingawa 25 ya hizi aliingia kama mchezaji mbadala.Hata hivyo,alimaliza msimu akiwa mshambulizi wa pili katika orodha ya timu akiwa na mabao 6.

Mchezo wake mzuri katika msimu huo ilimfanya ateuliwe katika kikosi cha Ghana,miaka tatu baada ya kucheza katika timu ya taifa kwa mara ya kwanza.Alichezea timu ya taifa katika mechi tatu lakini hakuteuliwa katika timu ya watu 23 waliocheza katika Shindano la Kombe la Dunia 2006.

Agyemang alicheza sana kama mchezaji mbadala katika misimu yake ya kwanza Deepdale akiikngia katika nusu ya pili ya mechi.Majeraha yalipowapata wachezaji wa timu ya kwanza ,Agyemang alianza kuchezeshwa kutoka nusu ya kwanza katika mechi kadhaa za misimu ya 2006/07.Alifunga mabao kadhaa mojawapo ikiwa bao la ushindi dhidi ya West Bromwich Albion.

Wasifu wake akiwa Queens Park Rangers

hariri

Katika mwezi wa Januari 2008, Agyemang Alihamia QUeens Park Rangers(QPR) kutoka klabu ya Preston kwa bei ya takriban £ 100,000. Alifunga bao lake la kwanza akiwa QPR katika mechi dhidi ya Sheffield United katika mechi yake ya kwanza katika ligi.

Agyemang alinawiri sana akiwa QPR na akafunga mabao matatu katika mechi tatu ya ligi, takwimu ambayo hajapita katika mechi zake zote zingine.

Baada ya kushindwa 3-1 na timu ya Watford, mnamo tarehe 7 Desemba 2009, Aygemang ,iliripotiwa ilibidi amzuie meneja wa klabu, Jim Magilton, baada ya kumpiga kwa kichwa Akos Buzsaky.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Agyemang alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Ghana katika mechi dhidi ya Nigeria mnamo 30 Mei 2003 katika Shindano la Kombe la LG,lilioandaliwa na Nigeria. Alifunga bao baada ya dakika tatu tu.Ghana , ingawaje , walishindwa 3-1. Alicheza katika mechi za kirafiki za kabla ya Shindano la Kombe la Dunia dhidi ya Mexico mnamo 1 Machi 2006. Hata hivyo alipoteza nafasi katika timu ya Ghana iliyocheza katika Shindano hilo.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri