Paul Victor Obeng
Paul Victor Obeng anajulikana kama PV Obeng (19 Agosti 1947 [1] - 17 Mei 2014) alikuwa mhandisi wa mitambo na mwanasiasa kutoka Ghana . Alikuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah . [2] Mnamo 2010, aliteuliwa na Rais John Atta Mills kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Mipango ya Maendeleo (NDPC) . Hadi kifo chake, alikuwa Mshauri Mkuu wa Raisi wa John Dramani Mahama. [3] [4] Alihudumu chini ya Rais Jerry John Rawlings, John Evans Atta Mills na John Dramani Mahama kwa nyadhifa tofauti. Alikuwa mjumbe na katibu mratibu na mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu wa Baraza la Muda la Kitaifa la Ulinzi. [5] [6] Alifariki tarehe 17 Mei 2014. [7]
Maisha binafsi
haririPaul Victor Obeng aliooana na Rose Obeng na walikuwa na watoto wanne. [8] Alikuwa Mkristo na aliabudu kama Mkatoliki wa Kirumi . [9] Baada ya kifo chake, mke wake Rose alitoa kumbukumbu ya marehemu mume na kumuelezea kama
'' mtu mwenye sifa nyingi, mwenye kipaji, mchapakazi, asiye na ubinafsi, mwanadiplomasia, lakini mnyenyekevu '' . [10]
Marejeo
hariri- ↑ "Paul Victor Obeng (PV) | Profile | Africa Confidential". www.africa-confidential.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-15.
- ↑ "P. V. Obeng Advocates Strong Public/Private Universities Partnership". www.theheraldghana.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-27. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Anane, Ernest Best (22 Agosti 2013). "PV Calls For Accountability In Sanitation & Water Delivery". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Ghanaian Chronicle (Accra). Iliwekwa mnamo 15 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mahama remembers late Paul Victor Obeng". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). 2018-05-18. Iliwekwa mnamo 2021-02-15.
- ↑ Sub-Saharan Africa Report (kwa Kiingereza). Foreign Broadcast Information Service. 1984.
- ↑ Ghana, Two Years of Transformation, 1982-1983 (kwa Kiingereza). Information Services Department. 1984.
- ↑ Osam, Efua Idan (17 Mei 2014). "Gov't confirms PV Obeng's death". Citi FM. Iliwekwa mnamo 15 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "PV Obeng goes home". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). 2014-08-16. Iliwekwa mnamo 2021-02-14.
- ↑ "PV Obeng laid to rest in hometown - MyJoyOnline.com". www.myjoyonline.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-02-14.
- ↑ "News & Event | NDPC". www.ndpc.gov.gh. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-04. Iliwekwa mnamo 2021-02-15.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paul Victor Obeng kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |